Qadariyyah wanakanusha makadirio. Nao ni Mu´tazilah. Wanaona kuwa matendo ya waja wameyaumba wao wenyewe, Allaah hakuyataka wala hakuyaumba. Kwa ajili hiyo wakaitwa “waabudia moto wa ummah huu”[1]. Waabudia moto wanaamini kuwepo kwa waumba wawili: muumbaji wa kheri na muumbaji wa shari. Kuhusu Qadariyyah wamethibitisha waumbaji wengi pamoja na Allaah.

Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) amesema:

“… na wengine wote ambao wanaenda kinyume na Sunnah na mkusanyiko na wakakumbatia upotofu.”

Bi maana mapote mengine yote ya upotofu yaliyoenda kinyume na Qur-aan na Sunnah.

[1]Abu Daawuud (4691). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniykatika ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (4691).

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 265-266
  • Imechapishwa: 27/05/2025