Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

172 – Hii ndio dini na ´Aqiydah yetu, kwa nje na kwa ndani.

173 – Sisi tunajitenga mbali kutokana na ambaye anaenda kinyume na yale yote tuliyoyataja na kuyabainisha.

174 – Tunamuomba Allaah (Ta´ala) atuthibitishe juu ya imani na atufishe katika hali hiyo.

MAELEZO

Yote tuliyoyataja katika kitabu hichi cha  ´Aqiydah ndio dini yetu sisi waislamu. Sisi tunajitenga mbali na kila ambaye anaenda kinyume nayo. Kwa sababu ni ´Aqiydah ya haki na yale yote yanayoenda kinyume nayo ni ya batili.

Baada ya mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) kubainisha ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, akafanya adabu na Allaah na akamuomba amfanye imara juu yake. Haitoshi kwa mtu akaitambua ´Aqiydah. Mwanachuoni anaweza kutekeleza na kukosea. Kamwe mtu asidanganyike kwa elimu yake na akajihisi salama kutokana na mitihani. Je, elimu yake inalingana na elimu ya Ibraahiym (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Yeye ndiye alisema:

رَبِّ اجْعَلْ هَـٰذَا الْبَلَدَ آمِنًا وَاجْنُبْنِي وَبَنِيَّ أَن نَّعْبُدَ الْأَصْنَامَ رَبِّ إِنَّهُنَّ أَضْلَلْنَ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ

“Ibraahiym aliposema: “Ee Mola wangu! Ufanye mji huu uwe wa amani na unikinge mimi na wanangu kuabudu masanamu.” Ee Mola wangu! Hakika hao wamepoteza wengi kati ya watu.”[1]

Mtu anatakiwa kumuomba Allaah usalama. Ni wanazuoni wangapi wametekeleza na kupinda kutokana na dini! Matendo yanazingatiwa ule mwisho wake.

[1] 14:35-36

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 262-263
  • Imechapishwa: 27/05/2025