Miongoni mwa madhara makubwa ya kuacha kuswali na viatu ni kwamba waislamu wengi wamekuwa ni wajinga juu ya Sunnah hii. Wanaona kuwa yule ambaye anaswali na viatu vyake ametenda kosa kubwa na wanamuona sawa na wale ambao wamefanya uhalifu mkubwa. Yemen nimemsikia mlinzi mmoja wa msikiti akisema:
“Kuna mtu aliyetoka Saudi Arabia kisha akarudi nchini mwake na akataka kuingia msikitini. Nikamwambia endapo utaingia msikitini na viatu vyako nitakuvunja mguu wako.”
Bwana huyu anadai kuwa ni miongoni mwa wanazuoni licha ya kwamba ni mjinga juu ya madhehebu yake. ash-Shawkaaniy (Rahimahu Allaah) ameeleza kuhusu uwekwaji Shari´ah wa kuswali na viatu:
“Miongoni mwa ambao wameona kuwa inapendeza ni al-Haadawiyyah ingawa watu wa kawaida miongoni mwao wanaikataa. Imaam al-Mahdiy amesema katika ”al-Bahr”: ”Kuswali na viatu vilivyo safi kunapendekezwa kwa mujibu wa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): ”Swalini na viatu vyenu.”[1]
Niliona kundi la watu katika msikiti wa Haram ya Makkah wakimzunguka mtu mmoja chini ya kipaza sauti wakimkemea kwa sababu ya kuswali akiwa amevaa viatu. Mmoja wao akasema kuhusu mtu huyo ambaye anaswali na viatu vyake ya kwamba ni shaytwaan. Kwa masikitiko msemaji wa maneno hayo ni mmoja wa wanaochunga swalah za mkusanyiko Haram. Hakika kama angelijua kuwa ni Sunnah, basi asingethubutu kumwambia ndugu yake muislamu kuwa yeye ni ”shaytwaan”.
Bisha nilimwona mtu mwenye dalili za wema na kumcha Allaah akimkemea aliyekuwa akiswali na viatu vyake. Alipoambiwa kuwa ni Sunnah, akasema:
”Ninajikinga kwa Allaah dhidi ya Sunnah hii.”
Baya zaidi kuliko yote haya ni kwamba baadhi ya ndugu katika Uislamu walitaka kuifanyia kazi Sunnah hii katika mskiti wa Haram ya Madiynah, lakini watu waliwakemea kwa ukali sana, akachukuliwa na utawala na akaweka ahadi ya kutojirudia.
Haya yote yanatokana na wanazuoni kutoitekeleza Sunnah hii. Kama wangeitekeleza, basi tusingehitaji kukusanya Hadiyth hizi na kuzieneza kati ya watu. Sababu nyingine pia ni watu kupuuzilia mbali vitabu vya Sunnah. Kama watu wangerudi katika vitabu hivyo, basi wasingekuwa na shaka yoyote kuhusu usahihi wa kuswali kwa viatu na kwamba ni Sunnah iliyoamrishwa.
[1] Nayl-ul-Awtwaar (2/135).
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 25-26
- Imechapishwa: 19/06/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket