Kuna Hadiyth nyingi zinazounga mkono kupangusa juu ya viatu:
1 – Imaam Abu Daawuud amepokea katika ”as-Sunan” yake kutoka kwa Aws bin Abi Aws ath-Thaqafiy, ambaye ameeleza:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitawadha na akapangusa juu ya viatu vyake na juu ya miguu yake.”[1]
2 – Imaam Ahmad akapokea kwamba Aws bin Abi Aws amesema:
”Nilimwona baba yangu siku moja akitawadha, akapangusa juu ya viatu. Nikamwambia: ”Je, unapanguza juu yake?” Akasema: ”Hivi ndivyo nilivyomwona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akifanya.”[2]
3 – Imaam Ahmad pia amepokea kutoka kwa Aws aliyesema:
”Nilimwona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akitawadha ambapo akapangusa juu ya viatu vyake, kisha akasimama kwenda kuswali.”[3]
4 – Imaam Ibn Jariyr at-Twabariy amepokea katika tafsiri yake kutoka kwa Aws pia aliyesema:
”Nilimwona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akifika katika jaa la watu ambapo akatwawadha na akapangusa juu ya miguu yake.”
Kwa maana juu ya viatu vilivyokuwa juu ya miguu hiyo, ili iende sambamba na riwaya yake iliyotangulia[4].
5 – at-Twabaraaniy amesimulia kutoka kwa ´Abbaad bin Tamiym kutoka kwa baba yake aliyesema:
”Nilimwona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akitawadha ambapo akapangusa juu ya miguu yake.”[5]
6 – Imaam Ibn Jariyr at-Twabariy amepokea katika tafsiri yake kutoka kwa Hudhayfah ambaye amesema:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuja kwenye jaa la watu fulani ambapo akakojoa juu yake. Kisha akaomba maji, akatawadha na akapangusa juu ya viatu vyake.”[6]
[1] Abu Daawuud (160). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (160).
[2] Ahmad (12/475).
[3] Ahmad (12/473).
[4] Tafsiri bora zaidi ni kusema kwamba alipangusa juu ya viatu vyake na miguu yake. Kwa maana hiyo ndiyo inayoafikiana na riwaya ya kwanza kwa herufi zake.
Kisha tambua kwamba Hadiyth hizi tatu kwa hakika ni Hadiyth moja. Wapokezi wametofautiana katika matamshi yake, lakini maana inayokusudiwa ni moja, nayo ni kufaa kupangusa juu ya viatu, hata kama havikuambatana na soksi. Hii ni Hadiyth Swahiyh na waliyotajwa na mtunzi wa kitabu na wengineo kama vile at-Twayaalisiy (1113), Ibn Abiy Shaybah (1/190) na al-Bayhaqiy (1/286–287). Nimezungumzia cheni ya wapokezi wake katika ”Swahiyh Abiy Daawuud”.
[5] Ibn Khuzaymah pia ameipokea katika ”as-Swahiyh” yake (201). Wapokezi wake wote ni wneye kuaminika isipokuwa mwalimu wake Ibn Khuzaymah ambaye ni Abu Zuhayr ´Abdul-Majiyd bin Ibraahiym al-Miswriy, kwa hakika sikupata wasifu wake kama nilivyosema katika maelezo yangu juu yake. Huenda at-Twabaraaniy aliisimulia kwa njia nyingine isiyokuwa yake. Hata hivyo ”al-Mu´jam” yake iko nje ya uwezo wangu mpaka niweze kurejelea ipasavyo mlolongo wa wapokezi wake. Lakini tafsiri ya Hadiyth ni kama ile iliyotangulia; ni kwamba alipangusa juu ya viatu na miguu yake.
[6] Wapokezi wake ni wenye kuaminika, lakini Hadiyth hii ni yenye hali isiyo ya kawaida. Kwa sababu wapokezi waaminifu wenye kuhifadhi miongoni mwa wanafunzi wa al-A´mash waliisimulia kwa tamko ”soksi zake” badala ya ”viatu vyake”, kama alivyosema Ibn Jariyr at-Twabariy mwenyewe (10/78). Hii ndiyo iliyohifadhiwa na iliyopokelewa na al-Bukhaariy na Muslim. Yaliyotangulia na yatakayokuja yanatosha bila kuitaja zaidi.
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 43-44
- Imechapishwa: 08/04/2026

Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 43-44
Imechapishwa: 08/04/2026
https://firqatunnajia.com/24-mtume-wa-allaah-alipangusa-juu-ya-viatu-vyake/