Maneno yake katika Hadiyth:

“Amewaamrisheni swalah. Mnaposwali basi msigeuke, kwani hakika Allaah huelekeza uso Wake kwa uso wa mja wake katika swalah yake muda wa kuwa hajageuka.”

Kugeuka kunakokatazwa katika swalah ni aina mbili:

1 – Ni kugeuka kwa moyo kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall) kwenda kwa asiyekuwa Yeye.

2 – Ni kugeuka kwa macho.

Yote mawili yamekatazwa. Allaah haachi kumkabili mja Wake maadamu mja yuko makini katika swalah yake. Iwapo atageuka kwa moyo au kwa macho, basi Allaah (Ta´ala) humpuuza. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa kuhusu kugeuka kwa mtu katika swalah yake ambapo akasema:

“Ni wizi ambao shaytwaan anaiba kutoka katika swalah ya mja.”[1]

Katika masimulizi mengine Allaah husema:

“Je, kwa aliye bora kuliko Mimi? Je, kwa aliye bora kuliko Mimi?”

[1] al-Bukhaariy (751).

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 43
  • Imechapishwa: 05/08/2025