149 – Husayn bin Hasan bin Harb ametukhabarisha: ´Abdullaah bin al-Mubaarak ametukhabarisha, kutoka kwa Yuunus, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa ´Urwah na Sa´iyd bin al-Musayyab, ambao wameeleza kuwa Hakiym bin Hizaam ambaye:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) aliniambia: “Ee Hakim! Hakika dunia ni tamu na ya kijani kibichi.”[1]

150 – Ibn Kaasib amenikhabarisha ametukhabarisha mfano wa hayo: ´Abdullaah bin Wahb amenikhabarisha, kutoka kwa ´Amr bin al-Haarith, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa ´Urwah na Sa´iyd bin al-Musayyab, ambao wamehadithia kwamba Hakiym bin Hizaam amewakhabarisha kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

151 – ´Abbaas bin al-Waliyd an-Narsiy ametukhabarisha: Daawuud bin ´Abdir-Rahmaan al-´Attwaar ametukhabarisha, kutoka kwa Ismaa´iyl bin Umayyah, kutoka kwa Sa´iyd bin Abiy Sa´iyd, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hakika dunia hii ni tamu na ya kijani kibichi.”

152 – Ibn Hisaab ametukhabarisha: Hammaad bin Zayd ametukhabarisha, kutoka kwa Yahyaa bin Sa´iyd, kutoka kwa ´Umar bin Kathiyr bin Aflah, kutoka kwa ´Ubayd bin Sanuutwaa, kutoka kwa Khawlah bint Qays bin Qahd, ambaye ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Dunia ni tamu na ya kijani kibichi.”

153 – Ibn Kaasib ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Yaziyd ametukhabarisha, kutoka kwa Sa´iyd bin Abiy Ayyuub: Abul-Aswad ametukhabarisha, kutoka kwa an-Nu´maan bin Abiy ´Ayyaash az-Zarqiy, kutoka kwa Khawlah bint Thaamir al-Answaariyyah, ambaye ameeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema hayohayo.

154 – as-Saltw bin Mas´uud ametukhabarisha: Muhammad bin Khaalid bin Salamah al-Makhzuumiy ametukhabarisha: Baba yangu ametukhabarisha, kutoka kwa Muhammad bin ´Amr bin al-Haarith bin Abiy Dhwiraar, kutoka kwa mama yake madogo ´Amrah bint al-Haarith bin Abiy Dhiraar, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Dunia ni tamu na ya kijani kibichi.”

155 – Muhammad bin Ismaa´iyl ametukhabarisha: Bwana mmoja (ambaye amemtaja jina) ametukhabarisha: Hishaam bin ´Urwah ametukhabarisha, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ´Aaishah, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Dunia ni tamu na ya kijani kibichi.”

156 – Bakr bin Khalaf ametukhabarisha: ´Abdul-Wahhaab ametukhabarisha, kutoka kwa al-Muthannaa bin as-Swabbaah, kutoka kwa ´Amr bin Shu´ayb, kutoka kwa Sulaymaan bin Yasaar, kutoka kwa Maymuunah, mkewe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Dunia ni tamu na ya kijani kibichi.”

157 – Ya´quub bin Humayd ametukhabarisha: Anas bin ´Iyaadhw ametukhabarisha, kutoka kwa Abu Suhayl bin Maalik, kutoka kwa bwana mmoja ambaye amemuhadithia kutoka kwa Hudhayfah, kutoka kwa Anas, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

”Dunia ni tamu na ya kijani kibichi.”

[1] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (3410-3411).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 36-38
  • Imechapishwa: 06/07/2025