Swali 237: Ni ipi hukumu ya kutoa mawaidha kwa njia ya Khutbah wakati wa kumzika maiti?
Jibu: Sijui msingi wowote wa kutoa mawaidha wakati wa kumzika maiti kwa njia ya kwamba mtu akasimama kuwakhutubia na kuwakumbusha watu yanayompitikia mtu wakati wa kufa kwake na baada ya kuzikwa kwake. Haikuwa katika mwongozo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kusimama kama muhubiri makaburini akiwatolea watu mawaidha. Lakini ilikuwa inaweza kutokea wakati fulani akiwakumbusha maneno yanayonasibiana na hali halisi. al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kupitia kwa ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesema:
“Tulikuw katika makaburi ya al-Gharqad ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akatujilia akaketi chini na sisi tukakaa kumzunguka. Alikuwa na kijiti akaanza kuchimba nacho chini. Kisha akasema: ”Hakuna yeyote katika nyinyi isipokuwa yamekwishaandikwa makazi yake Peponi na makazi yake Motoni.” Wakasema: ”Ee Mtume wa Allaah! “Si tutegemee basi tuliyoandikiwa na tuache kutenda?” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Fanyeni matendo! Kwani hakika kila mmoja ni mwenye kufanyiwa wepesi juu ya kile alichoumbiwa. Kuhusu ambaye ni katika wenye furaha, atafanyiwa wepesi wa kufanya matendo ya wenye furaha. Kuhusu ambaye ni katika wala khasara atafanyiwa wepesi wa kufanya matendo ya wala khasara.” Kisha akasoma maneno Yake (Ta´ala):
فَأَمَّا مَنْ أَعْطَىٰ وَاتَّقَىٰ وَصَدَّقَ بِالْحُسْنَىٰ فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْيُسْرَىٰ وَأَمَّا مَن بَخِلَ وَاسْتَغْنَىٰ وَكَذَّبَ بِالْحُسْنَىٰ فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْعُسْرَىٰ
“Basi yule anayetoa na akamcha Allaah na akasadikisha lililo jema zaidi, basi tutamuwepesishia kwa yaliyo mepesi. Ama yule afanyaye ubakhili na akajiona amejitosheleza na akakadhibisha lililo jema zaidi, basi tutamuwepesishia kwa yaliyo magumu.”[1][2]
Imaam Ahmad na Abu Daawuud wamepokea kwamba al-Baraa´ bin ´Aazib (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Tulitoka pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika mazishi ya bwana mmoja kutoka katika Answaar. Tulipofika tukakuta mwanadani hajachimbwa. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaketi chini na sisi tukaketi pambizoni mwake. Ni kama kwamba walikuweko ndege juu ya vichwa vyetu. Mkononi alikuwa ameshika kijiti akipigapiga ardhini. Akainua kichwa na kusema: “Mtakeni ulinzi Allaah kutokamana na adhabu ya kaburi.” Alisema hivo mara mbili au mara tatu.”[3]
Hadiyth imetajwa katika “at-Targhiyb at-Tarhiyb”[4]. Haafidwh al-Mundhiriy amesema baada yake:
“Hadiyth ni nzuri. Wasimulizi wake ni wenye kutumiwa kama hoja katika as-Swahiyh.”
Kwa kufupisha ni kwamba haikupokelewa ni kwamba haikupokelewa kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisimama kama Khatwiyb akikiwaidhi watu.
[1] 92:05-10 al-Bukhaariy (4949) na Muslim (2647).
[2] al-Bukhaariy (1362) na Muslim (2647).
[3] Ahmad (4/287) na Abu Daawuud (4751).
[4] 4/365.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/234-236)
- Imechapishwa: 03/02/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/234-236)
Imechapishwa: 03/02/2026
https://firqatunnajia.com/237-ni-ipi-hukumu-ya-kutoa-mawaidha-kwa-njia-ya-khutbah-wakati-wa-kumzika-maiti/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket