Swali 235: Ni yepi yaliyowekwa katika Shari´ah kutoa mawaidha makaburini? Tumewasikia wenye kusema kuwa imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wengine wakasema kuwa ni Sunnah.
Jibu: Kusema kuwa haikupokelewa kabisa si sahihi. Na kusema pia kuwa ni Sunnah sio sahihi. Haikupokelewa kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisimama kwenye kaburi au makaburini wakati wa mchakato wa maziko na akiwatolea watu mawaidha na kuwakumbusha kana kwamba ni muhubiri wa siku ya ijumaa. Hato hatujayasikia. Kwa hiyo ni Bid´ah. Pengine huko mbele likaenda mbali zaidi. Huenda likapelekea yule mzungumzaji akaanza kumsema vibaya yule maiti na kutaja madhambi yake yaliyotangulia kama vile ya michezo na mzaha. Au pengine akamsema vibaya mfanya biashara fulani kwa mfano na kutaja makasiri yake aliokuwa nayo, magari na wafanyakazi wake na kwamba hivi sasa yuko ndani ya kaburi lake. Kwa ajili hiyo naona kuwa mtu asikhutubu makaburini. Kwa sababu sio katika Sunnah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya kumaliza kumzika maiti au anapokuwa anasubiri mchakato wa mazishi hakuwa anasimama na kuwakhutubia watu. Hatulitambui hili kutoka kwa wale waliotangulia wa mwanzo. Wao wako karibu zaidi na Sunnah kuliko sisi. Wala hatutambui kuwa wale makaliyfah waongofu walikuwa wakifanya hivo. Kutokana na ninavyojua sijui kuwa watu katika zama za Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan wala ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhum) walikuwa wakifanya hivo. Uongofu bora ni uongofu wa wale waliotangulia muda wa kuwa unaafikiana na haki.
Kuhusu maneno kwa njia ya maneno ya kwenye kikao hayana neno. Imethibiti ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitoka kwenda katika makaburi ya al-Baqiy´ na akawakuta watu wameketi chini wakisubiri mwanandani anayechimbwa kwa ajili ya kumzika bwana mmoja kutoka katika Answaar. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaketi chini na Maswahabah nao wakaketi karibu naye. Ndipo akaanza kuwasimulia hali ya mtu wakati anapokufa na hali ya mtu baada ya kuzikwa. Ilikuwa ni maongezi na sio kwa njia ya Khutbah[1]. Vilevile kuna wakati mwingine (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika mazishi mengine alisema:
”Hakuna yeyote katika nyinyi isipokuwa yamekwishaandikwa makazi yake Peponi na makazi yake Motoni.” Wakasema: ”Ee Mtume wa Allaah! “Si tutegemee basi tuliyoandikiwa na tuache kutenda?” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Fanyeni matendo! Kwani hakika kila mmoja ni mwenye kufanyiwa wepesi juu ya kile alichoumbiwa.”[2]
Kwa kifupisha ni kwamba mawaidha kwa njia ya kwamba mtu anasimama na kutoa Khutbah wakati wa mchakato wa maziko au baada yake sio katika Sunnah na ni jambo lisilotakikana. Hata hivyo kuketi pamoja na marafiki zake na akazungumza kwa njia inayonasibiana na maeneo hayo ni jambo zuri kwa ajili ya kumwigiliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
[1] Ahmad (4/287) na Abu Daawuud (4751).
[2] al-Bukhaariy (1362) na Muslim (2647).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/231-233)
- Imechapishwa: 03/02/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/231-233)
Imechapishwa: 03/02/2026
https://firqatunnajia.com/235-je-imesuniwa-kukuwaidhi-watu-makaburini/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket