Mnajimu ni yule ambaye anasimulia mambo yajayo huko mbele kwa kuziangalia nyota. Pindi kunapozuka nyota fulani, basi anadai kuwa kutatokea kitu fulani. Wakati inapopotea nyota fulani, basi anadai kuwa kutatokea jambo fulani. Wakati kunapoonekana buruji fulani wanatabiri kutokea kwa janga fulani, wakati kunapoonekana buruji fulani wanatabiri kutokea kwa furaha fulani. Namna hii matabiri yao yanategemea mambo haya ya uwongo. Unajimu ni kuyanasibisha matukio ya ardhi na hali za anga, kama alivyotambulisha jambo hilo Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah).
Unajimu ni miongoni mwa mambo kabla ya kuja Uislamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mambo manne katika ummah wangu ni katika mambo ya kipindi cha kishirikina na hawatoyaacha: kujifakharisha kwa ukoo, kutukana nasaba, kuomba mvua kupitia nyota na maombelezo kwa wafu.”[1]
Bi maana kuomba mvua kupitia nyota. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
فَلَا أُقْسِمُ بِمَوَاقِعِ النُّجُومِ وَإِنَّهُ لَقَسَمٌ لَّوْ تَعْلَمُونَ عَظِيمٌ إِنَّهُ لَقُرْآنٌ كَرِيمٌ فِي كِتَابٍ مَّكْنُونٍ لَّا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ تَنزِيلٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ أَفَبِهَذَا الْحَدِيثِ أَنتُم مُّدْهِنُونَ وَتَجْعَلُونَ رِزْقَكُمْ أَنَّكُمْ تُكَذِّبُونَ
“Basi Naapa kwa maangukio ya nyota – na hakika hicho ni kiapo kikubwa mno, lau mngelielewa! – hakika hii bila shaka ni Qur-aan karimu, katika Kitabu kilichohifadhiwa, hakuna akigusaye isipokuwa waliotakaswa, ni uteremsho kutoka kwa Mola wa walimwengu! Je, kwa maneno haya nyinyi ni wenye kuitweza na kuikanusha na mnafanya shukurani za riziki yenu kuwa nyinyi mnakadhibisha… “[2]
Mnathubutuje kunasibisha zile riziki mnazopata kwa nyota na hali za anga? Haya ni miongoni mwa ´Aqiydah za kipindi kabla ya kuja Uislamu. Nyota ni kiumbe katika viumbe vya Allaah zinazoendeshwa, ambazo Allaah ameziumba kwa ajili ya mambo matatu:
1 – Zinaipamba dunia ya chini.
2 – Ni vimondo kwa mashaytwaan.
3 – Alama ambazo mtu anaongozwa kwazo katika visa vya baharini na nchikavu.
Ambaye ataona kuwa zina malengo mengine basi amekula patupu. Ukiizingatia Qur-aan basi utaona kuwa Allaah ametaja kuwa nyota zina faida tatu. Kuhusu yale mambo mbalimbali yanayozuka ardhini nyota hazina chochote kuhusiana nayo. Hakika hapana vyengine wanajimu wanawadanganya na kuwatia watu mchanga wa machoni pindi wanapodai matukio mbalimbali ni kwa sababu ya nyota. Allaah (Subhaanah) amesema:
وَسَخَّرَ لَكُمُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ ۖ وَالنُّجُومُ مُسَخَّرَاتٌ بِأَمْرِهِ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ
”Amekutiishieni usiku na mchana na jua na mwezi. Na nyota zimetiishwa kwa amri Yake. Hakika bila shaka katika hayo kuna alama kwa watu wanaotia akilini.”[3]
Mambo haya yaliyotajwa hapo juu yanaitia kasoro ´Aqiydah na kuibatilisha imani yake pale atakaposadikisha kuwa nyota ndizo ambazo zimefanya mambo hayo katika ulimwengu.
Hatumsadikisha yeyote ambaye anaenda kinyume na Qur-aan, Sunnah au maafikiano. Mambo haya matatu yameegemea juu ya dalili – na kila kinachoenda kinyume nayo – ni mamoja katika maneno, matendo au imani – ni batili.
[1] Muslim (934).
[2] 56:75-82
[3] 16:12
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 252-253
- Imechapishwa: 06/05/2025

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 252-253
Imechapishwa: 06/05/2025
https://firqatunnajia.com/231-unajimu-na-nyota/