Kuhusu Moto ni makaazi ya uchafu katika maneno, matendo, vyakula na vinywaji. Allaah (Ta´ala) amesema:
لِيَمِيزَ اللَّـهُ الْخَبِيثَ مِنَ الطَّيِّبِ وَيَجْعَلَ الْخَبِيثَ بَعْضَهُ عَلَىٰ بَعْضٍ فَيَرْكُمَهُ جَمِيعًا فَيَجْعَلَهُ فِي جَهَنَّمَ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ
”… ili Allaah apambanue waovu na wema kisha aweke waovu juu ya waovu wengine, halafu awarundike pamoja awatie katika Moto wa Jahannam – hao ndio waliokhasirika.”[1]
Ni makaazi ya wachafu. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) huwakusanya wachafu wote pamoja ambapo huwawekea juu ya wenzao kama kitu kinachorundikwa juu ya kingine, kisha huwaweka wote humo Motoni pamoja na watu wake. Hakika ndani yake hakuna isipokuwa wachafu.
Hali ilivyokuwa kwamba watu wamegawanyika msafi ambaye hana uchafu wowote, mchafu ambaye hana twahara yoyote ndani yake na wa kati kati ambaye ana uchafu na usafi, basi makaazi yao yakawa matatu: makaazi ya walio safi kabisa, makaazi ya wachafu kabisa na walisoalia wasafi na wachafu, basi makaazi yao pia yakawa matatu tofauti: wakaazi ya wasafi watupu, makaazi ya wachafu watupu. Makaazi haya mawili hayateketei. Makaazi ya tatu ni ya wale wenye uchafu na usafi. Haya ndio makaazi yatayoteketea na ya wale watenda madhambi. Hakuna mpwekeshaji yeyote mtenda dhambi ambaye atabakia Motoni. Baada ya wao kuadhibiwa kwa kiwango cha dhambi zao watatolewa Motoni na kuingizwa Peponi. Hakutobaki isipokuwa makaazi ya wale wasafi watufupu na makaazi ya wachafu watupu.
[1] 8:37
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 42-43
- Imechapishwa: 05/08/2025
Kuhusu Moto ni makaazi ya uchafu katika maneno, matendo, vyakula na vinywaji. Allaah (Ta´ala) amesema:
لِيَمِيزَ اللَّـهُ الْخَبِيثَ مِنَ الطَّيِّبِ وَيَجْعَلَ الْخَبِيثَ بَعْضَهُ عَلَىٰ بَعْضٍ فَيَرْكُمَهُ جَمِيعًا فَيَجْعَلَهُ فِي جَهَنَّمَ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ
”… ili Allaah apambanue waovu na wema kisha aweke waovu juu ya waovu wengine, halafu awarundike pamoja awatie katika Moto wa Jahannam – hao ndio waliokhasirika.”[1]
Ni makaazi ya wachafu. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) huwakusanya wachafu wote pamoja ambapo huwawekea juu ya wenzao kama kitu kinachorundikwa juu ya kingine, kisha huwaweka wote humo Motoni pamoja na watu wake. Hakika ndani yake hakuna isipokuwa wachafu.
Hali ilivyokuwa kwamba watu wamegawanyika msafi ambaye hana uchafu wowote, mchafu ambaye hana twahara yoyote ndani yake na wa kati kati ambaye ana uchafu na usafi, basi makaazi yao yakawa matatu: makaazi ya walio safi kabisa, makaazi ya wachafu kabisa na walisoalia wasafi na wachafu, basi makaazi yao pia yakawa matatu tofauti: wakaazi ya wasafi watupu, makaazi ya wachafu watupu. Makaazi haya mawili hayateketei. Makaazi ya tatu ni ya wale wenye uchafu na usafi. Haya ndio makaazi yatayoteketea na ya wale watenda madhambi. Hakuna mpwekeshaji yeyote mtenda dhambi ambaye atabakia Motoni. Baada ya wao kuadhibiwa kwa kiwango cha dhambi zao watatolewa Motoni na kuingizwa Peponi. Hakutobaki isipokuwa makaazi ya wale wasafi watufupu na makaazi ya wachafu watupu.
[1] 8:37
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 42-43
Imechapishwa: 05/08/2025
https://firqatunnajia.com/23-moto-wa-milele-moto-wa-muda/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket