4 – Kugusa mwanamke kwa matamanio: Kumgusa mwanamke kwa matamanio. Hili ndilo alilolichagua Shaykh na ni moja kati ya mitazamo mitatu kuhusu suala hili. Maoni ya pili ni kwamba kumgusa mwanamke kunachengua wudhuu´ moja kwa moja. Maoni ya tatu ni kwamba kumgusa mwanamke hakuchengui wudhuu´ moja kwa moja, ni mamoja mtu amefanya hivo kwa matamanio au ni pasi na matamanio alimradi hakuna kitu kilichotoka kwa sababu ya matamanio hayo. Maoni haya ya mwisho ndio sahihi zaidi kwa kuwa hakuna kilichothibiti kuwa kugusa kunabatilisha. Tazama ”Fataawaa” (10/132–138) ya Shaykh Ibn Baaz (Rahimahu Allaah).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 23-24
  • Imechapishwa: 26/05/2026