Wakati wa kuomba du´aa moyo huhisi unyenyekevu, kujivunjavunja mbele ya Allaah na kuonyesha ile haja yake kubwa kwa ajili ya Allah (‘Azza wa Jall). Kadiri na uombaji na hitajio la mwombaji, ndio kunakuwa na uwezekano mkubwa wa kuitikiwa. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
“Mwombeni Allaah hali ya kuwa ni wenye yakini ya kuitikiwa. Kwani hakika Allaah haitiki du´aa kutoka kwenye moyo uliyoghafilika na wenye kupumbaa.”[1]
Ameipokea Ahmad na at-Tirmidhiy.
Miongoni mwa hayo ni kudhihirisha udhalilifu wakati wa kuuliza na kuomba pamoja na kuomba kwa kung´ang´ania. al-Awzaa’iy (Rahimahu Allaah) amesema:
“Ilikuwa inasemwa kwamba du´a bora kabisa ni kule kuomba kwa kung´ang´ania na kumnyenyekea.”
Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhumaa) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) aliomba siku ya ´Arafah na akasema:
“Ee Allaah, hakika Wewe unaona mahali pangu, unasikia maneno yangu na hakuna kinachojificha Kwako kutokana na hali yangu. Mimi ni mnyonge na fakiri, mwenye kuomba msaada na mwenye kuomba hifadhi, mwenye khofu na mwenye wasiwasi, mwenye kukiri na kukubali dhambi yake. Ninakuomba kama masikini na nakuomba kama mtenda dhambi mtwevu. Nakuomba du´aa ya mwenye khofu na mwenye dhiki, du´aa ya ambaye shingo yake inanyenyekea Kwako, ambaye mwili wake umenyenyekea Kwako, ambaye uso wake umenyenyekea Kwako, ambaye macho yake yana machozi kwa ajili Yako. Ee Allaah! Usinifanye ni mwenye kutoitikiwa. Kuwa kwangu ni mwenye huruma na mpole na mwenye kunirehemu. Wewe ndiye mbora wa wanaoulizwa, Wewe ndiye mbora wa watoaji.”[2]
Ameipokea at-Twabaraaniy.
Baadhi yao walikuwa wakisema katika du´aa zao:
“Naapa kwa utukufu Wako na udhalilifu wangu, naapa kwa mali Yako na ufukara wangu.”
Twaawuus (Rahimahu Allaah) amesema:
“Usiku mmoja `Aliy bin al-Husayn (Rahimahu Allaah) aliingia nyumbani kwangu ambapo akaanza kuswali. Nikamsikia akisema katika Sujuud yake: “Mimi ni mja Wako mdogo katika kutoweka kwako, masikini Wako katika kutoweka kwako, fakiri Wako katika kutoweka kwako, mwombaji Wako katika kutoweka kwako.” Nilihifadhi jumla hizo. Sijawahi kuziomba wakati wa dhiki isipokuwa nilisahilishiwa.”
Ameipokea Ibn Abiyd-Dunyaa.
Ibn Baakuuyah as-Suufiy (Rahimahu Allaah) amesimulia kwamba kuna mfanya ´ibaadah mmoja, ambaye alihiji mara themanini kwa miguu, wakati alipokuwa akifanya Twawaaf akasema:
“Ee Mpenzi!” Tahamaki akasikia sauti ikisema: “Je, huridhiki kuwa masikini na hivyo uwe mpenzi wangu?” Bwana yule akasema: “Nikapoteza fahamu. Baada ya hapo nilikuwa nikisema: “Mimi ni maskini Wako na natubia kwa kusema kwangu ‘mpenzi wangu.”
[1] Ahmad (6653), at-Tirmidhiy (3479), at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Awsatw” (5109) na al-Haakim (1817). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ul-Jaamiy´” (245).
[2] at-Twabaraaniy (11/174). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf-ul-Jaamiy´” (1186).
- Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Hanbaliy (afk. 795)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Khushuu´ fiys-Swalaah, uk. 85-88
- Imechapishwa: 24/11/2025

Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Hanbaliy (afk. 795)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Khushuu´ fiys-Swalaah, uk. 85-88
Imechapishwa: 24/11/2025
https://firqatunnajia.com/23-haja-na-kujidhalilisha-kwa-moyo-wakati-wa-kuomba-duaa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket