22. Ni wanachuoni wepi unaowapendekezea wanafunzi kusoma kwao?

Swali 22: Ni wepi watu wa Da´wah as-Salafiyyah katika mji wetu wa Saudi Arabia ambao inatakiwa kusoma kwao?

Jibu: Wanachuoni wa Salafiyyah ambao darsa zao zinatakiwa kusikilizwa ni pamoja na wafuatao:

1 – Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

2 – Shaykh Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan

3 – Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh

4 – Shaykh ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Ghudayyaan

Na wanachuoni wengine wote katika Kibaar-ul-´Ulumaa´. Kadhalika wanachuoni waliyopo al-Madiynah na wanachuoni wengine ambao inabainika kwao kuinusuru haki na kupambana na u-Hizbiyyah. Matendo yao haya ni dalili tosha kuwa ni Salafiyyuun. Hivyo, inatakikana kukaa kwao, kusikiliza kanda zao, darsa zao na halaka zao. Mambo yanatakiwa kuwa namna hii.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah
  • Imechapishwa: 23/07/2017