92 – ´Ubaydullaah bin Abiyl-Fath al-Faarisiy amenikhabarisha: Muhammad bin al-´Abbaas al-Khazzaaz ametuzindua: Ja´far bin Muhammad as-Swandaliy ametuhadithia: al-Hasan bin Muhammad bin as-Swabbaah ametukhabarisha: Muhammad bin Yaziyd bin Khunays ametuhadithia: ´Umar bin Qubays amesema: ´Atwaa’ ametuhadithia:

”Alikuwepo kijana mmoja alikuwa akienda kwa mama wa Waumini ´Aaishah kumuuliza maswali ambapo akimjibu. Siku moja, alipokuja kumuuliza, akamwambia: ”Ee mwanangu kipenzi! Umeshayafanyia kazi yale uliyosikia kutoka kwangu?” Akasema: ”Hapana, naapa kwa Allaah, ee mamangu kipenzi!” Akasema: ”Ee mwanangu kipenzi! Ni kwa nini unajizidshia hoja ya Allaah dhidi yetu na dhidi yako?”

93 – al-Hasan bin Muhammad al-Khallaal amenihadithia: ´Umar bin Ibraahiym bin Kathiyr al-Muqri’ ametuhadithia: Ja´far bin Muhammad as-Swandaliy ametuhadithia: Abu Hafsw ´Umar, mpwa wa Bishr bin al-Haarith, ametuhadithia: Nimemsikia Bishr akisema: al-Fudhwayl akisema:

”Ni bora kwa mtu asisikie Hadiyth hii kuliko aisikie kisha asiitendee kazi.”

94 – Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy bin Yazdaad al-Qaari’ ametukhabarisha: Abu Muhammad ´Abdullaah bin Muhammad bin Ja´far bin Hayyaan al-Aswbahaaniy ametukhabarisha nayo: Muhammad bin Yahyaa – yaani Ibn Mandah – ametuhadithia: Muhammad bin ´Iswaam ametuhadithia, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Abu Haazim, aliyesema:

”Watu wanaridhia matendo yanayotokana na elimu na wanaridhia matendo yanayotokana na maneno.”

95 – Muhammad bin Ahmad bin Rizq ametukhabarisha: ´Uthmaan bin Ahmad ad-Daqqaaq ametuzindua: Hanbal bin Ishaaq ametuhadithia: Abu ´Abdillaah – yaani Ahmad bin Hanbal – amenihadithia: Abu Qatwan ametuhadithia: Nimemsikia Ibn ´Awn akisema:

”Natamani isiwe ni hoja kwangu wala dhidi yangu.”

Bi maana elimu.

96 – Abu Qatwan amesimulia kuwa Shu´bah amesema:

”Hakuna kitu kingine nimekishikilia ambacho nachelea kisiniingize Motoni.”

97 – Muhammad bin Abiy Naswr an-Nursiy ametukhabarisha: Muhammad bin ´Abdillaah bin al-Husayn ad-Daqqaaq ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Muhammad bin ´Abdil-´Aziyz ametukhabarisha: Muhammad bin Ziyaad bin Farwah al-Baladiy ametuhadithia: Abu Shihaab ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin ´Abdillaah, kutoka kwa al-Qaasim bin ´Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Ibn Mas´uud, aliyesema:

”Nadhani kuwa mja anasahau elimu, aliyokuwa akiijua, kutokana na dhambi aliyoitenda.”

98 – Abu ´Abdillaah Ahmad bin ´Abdillaah bin al-Husayn bin Ismaa´iyl al-Mahaamiliy ametukhabarisha: ´Abdur-Rahmaan bin al-´Abbaas bin ´Abdir-Rahmaan bin Zakariyyaa al-Bazzaaz ametuhadithia: Muhammad bin Ibraahiym bin Hamduud al-Khazzaaz ametuhadithia: ´Abdullaah – yaani Ibn Abiy Ziyaad – ametuhadithia: Sayyaar ametuhadithia, kutoka kwa Ja´far, kutoka kwa Maalik, aliyesema:

”Nimesoma ndani ya Tawraat: “Iwapo mwanachuoni hatoifanyia kazi elimu yake huondoka ndani ya mioyo kama jinsi ambavo tone linateleza kwenye jiwe laini.”

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 60-62
  • Imechapishwa: 13/05/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy