7- Kujitenga mbali na vyama na makundi ya Kiislamu ya kisiri
Kama mnavyoona wenyewe kumejitokeza makundi yenye kujitenga na kundi la waislamu lililowekwa katika Shari´ah kutokana na zile fikira na mipangilio walionayo. Makundi yote haya yamekusanyika juu ya lengo moja: kuchukia jamii ya Kiislamu inayokubalika katika Shari´ah na kuitazama kwa aina ya jamii ya kipindi cha kikafiri. Mara nyingi wanakuwa na mtazamo huu na wanaonelea hivi.
Miongoni mwa makundi yenye mtazamo huo ni kundi la al-Ikhwaan al-Muslimuun, Jamaa´at-ut-Tabliygh na Hizb-ut-Tahriyr.
Nasema kwa masikitiko makubwa wako ambao wameifanya Salafiyyah kuwa ni kipote kama mapote haya. Kama ambavo pia wanapatikana wanaojaribu kuifanya Salafiyyah kama mapote haya. Tunajilinda kwa Allaah (Ta´ala) kutokamana na kitendo hichi na shari za mwenye kufanya hivo. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
“Kuhusu manasibisho yanayofarikisha kati ya waislamu na ndani yake kuna kutoka nje ya mkusanyiko na kupelekea katika mpasuko na kupita njia za kizushi na kufarikisha Sunnah na ufuataji, ni mambo yaliyokatazwa na anapata dhambi anayefanya hivo. Aidha anatoka nje ya kumtii Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[1]
Allaah ndani ya Kitabu Chake ametuita waislamu. Imethibiti katika “Musnad Imaam Ahmad” kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yule mwenye kuita katika wito wa kipindi cha kikafiri basi ni katika watu wa Motoni.” Bwana mmoja akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Hata kama anafunga na kuswali?” Akajibu: “Ndio, ingawa anafunga na kuswali. Lakini jiiteni kwa jina la Allaah ambalo amekuiteni ´waja wa Allaah waislamu waumini`.”[2]
[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (11/514).
[2] Ahmad katika ”Musnad” (37/543) (22910).
- Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Usuwl-ud-Da´wah as-Salafiyyah, uk. 56-57
- Imechapishwa: 18/08/2020

Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Usuwl-ud-Da´wah as-Salafiyyah, uk. 56-57
Imechapishwa: 18/08/2020
https://firqatunnajia.com/22-msingi-wa-saba-kujitenga-mbali-na-uyamavyama-na-ukundikundi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)