22. Hadiyth ”Ikiwa mmoja wenu atakanyaga uchafu na viatu vyake… ”

Abu Daawuud (1/148) amesema: Ahmad bin Ibraahiym ametuhadithia: Muhammad bin Kathiyr (as-Swan´aaniy) ametuhadithia, kutoka kwa al-Awzaa´iy, kutoka kwa Ibn ´Ajlaan, kutoka kwa Sa´iyd bin Abiy Sa´iyd, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

”Ikiwa mmoja wenu atakanyaga uchafu na viatu vyake, basi kusafika kwake ni mchanga.”[1]

Ameipokea Ibn Khuzaymah (1/148), Ibn Hibbaan, uk. 85 katika “Mawaarid-udh-Dhwamaan”, al-Haakim (1/11), ambaye amesema kwamba ni “Swahiyh kwa mujibu wa sharti za Muslim”, al-Bayhaqiy (2/430) na Ibn Hazm katika “al-Muhallaa” (1/93)[2].

[1] Abu Daawuud (386). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (386).

[2] Faida. Abut-Twayyib amesema katika “´Awn-ul-Ma´buud”:

”Ijapo Muhammad bin Kathiyr ni dhaifu, amefanyiwa ufuatiliwaji na Abul-Mughiyrah, al-Waliyd bin Maziyd na ´Umar bin ´Abdil-Waahid, kutoka kwa al-Awzaa´iy. Wote ni wenye kuaminika. Hata kama baadhi wamemdhoofisha Muhammad bin ´Ajlaan, wengi wamemzingatia kuwa ni mwenye kuaminika.”

Kisha akataja Hadiyth zinazotilia nguvu.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 23
  • Imechapishwa: 19/06/2025