22- al-Qaadhwiy al-Husayn bin Ismaa´iyl ametuhadithia: Yuusuf bin Muusa al-Qattwaan ametuhadithia: Abu Mu´aawiyah ametuhadithia, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa ´Alqamah, kutoka kwa ´Abdullaah aliyesema:
“Kuna mwanamume kutoka katika watu wa Kitabu alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ee Abul-Qaasim! Je, imekufikia kwamba Allaah (´Azza wa Jall) atabeba mbingu kwenye kidole, ardhi kwenye kidole, viumbe kwenye kidole na ardhi kwenye kidole?” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaanza kucheka mpaka magego yake yakaonekana na Allaah akateremsha:
وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ
“Hawakumkadiria Allaah vile inavyostahiki kumkadiria na hali ardhi yote itakamatwa mkononi Mwake siku ya Qiyaamah na mbingu zitakunjwa mkononi Mwake wa kuume. Ametakasika na upungufu na yu juu kabisa kuliko yale wanayomshirikisha.”[1]
Jariyr amesema katika Hadiyth yake:
“Milima na miti kwenye kidole, maji na ardhi kwenye kidole na viumbe wengine wote kwenye kidole.”
[1] 39:67
- Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 58-60
- Imechapishwa: 05/11/2017
22- al-Qaadhwiy al-Husayn bin Ismaa´iyl ametuhadithia: Yuusuf bin Muusa al-Qattwaan ametuhadithia: Abu Mu´aawiyah ametuhadithia, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa ´Alqamah, kutoka kwa ´Abdullaah aliyesema:
“Kuna mwanamume kutoka katika watu wa Kitabu alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ee Abul-Qaasim! Je, imekufikia kwamba Allaah (´Azza wa Jall) atabeba mbingu kwenye kidole, ardhi kwenye kidole, viumbe kwenye kidole na ardhi kwenye kidole?” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaanza kucheka mpaka magego yake yakaonekana na Allaah akateremsha:
وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ
“Hawakumkadiria Allaah vile inavyostahiki kumkadiria na hali ardhi yote itakamatwa mkononi Mwake siku ya Qiyaamah na mbingu zitakunjwa mkononi Mwake wa kuume. Ametakasika na upungufu na yu juu kabisa kuliko yale wanayomshirikisha.”[1]
Jariyr amesema katika Hadiyth yake:
“Milima na miti kwenye kidole, maji na ardhi kwenye kidole na viumbe wengine wote kwenye kidole.”
[1] 39:67
Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 58-60
Imechapishwa: 05/11/2017
https://firqatunnajia.com/22-dalili-juu-ya-mkono-wa-allaah-8/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)