Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

164 – Hatumfadhilishi yeyote katika mawalii juu ya yeyote katika Manabii. Tunasema kuwa Nabii mmoja ni bora kuliko mawalii wote.

MAELEZO

Mtunzi (Rahimahu Allaah) amehama kutoka kwa wanazuoni kwenda kwa mawalii. Uwalii ni ukaribu na mapenzi. Mawalii wako karibu na wanapendwa na Allaah (´Azza wa Jall), na ndio maana wakaitwa hivyo. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ

“Hakika Allaah anawapenda wenye kutubia na anawapenda wenye kujitwaharisha.”[1]

إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ

“Hakika Allaah anapenda wafanyao ihsaan.”[2]

Allaah amewabainisha pale aliposema:

أَلَا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّـهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ

“Tanabahi! Hakika mawalii wa Allaah hawana khofu juu yao na wala hawatohuzunika. Ambao wameamini na wakawa wanamcha.”[3]

Ili mtu aweze kuwa walii ni lazima akusanye sifa mbili, imani na kumcha Allaah.

[1]2:222

[2]02:195

[3]10:62-63

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 238-239
  • Imechapishwa: 28/04/2025