Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
159 – Tunathibitisha ukhalifah baada ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wa kwanza ni Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anhum), ambaye alifadhilishwa na kutangulizwa kabla ya ummah mzima, kisha ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh), kisha ´Uthmaan bin ´Affaan (Radhiya Allaahu ´ann) na kisha ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh). Hawa ndio makhaliyfah waongofu na maimamu wenye kuongoza.
MAELEZO
Alipomaliza kutaja yale yanayopasa juu ya Maswahabah katika mapenzi na urafiki, kuacha kuwachukia na kumchukia ambaye anawachukia na kutoingia yale ile mizozo iliotokea kati yao, ndipo akaingia kutaja ukhalifah baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni kwa mpangilio aliyotaja. Mwishoni mwa uhai wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kabla ya yeye kufa, alimtanguliza Abu Bakr mbele awaswalishe watu. Hapa kuna maashirio ya ukhalifah wake. Ndio maana Maswahabah wakasema wakati walipompa kiapo cha usikivu:
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekuridhia juu ya dini yetu; je, tusikuwie radhi juu ya dunia yetu?”
Hivyo wakampa kiapo cha usikivu. Isitoshe Abu Bakr alikuwa na fadhilah kubwa kabla na baada ya kuhajiri. Yeye ndiye mtu ambaye alikuwa na haki zaidi baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Baada yake anafuatia ´Umar bin al-Khattwaab, ambaye aliteuliwa na mtangulizi wake Abu Bakr. Kisha anafuatia ´Uthmaan, kwa maafikiano ya Maswahabah kutokana na uchaguzi wa watu wa mashauriano – baraka lililojumuisha wale Maswahabah kumi wabora waliobashiriwa Pepo ambao waliteuliwa na ´Umar. Baada ya kuuliwa ´Uthmaan akachukua ukhalifah ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh). Huu ndio mpangilio wa ukhalifah. Yule mwenye kudai kuwa ukhalifah, baada ya kufariki kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ulitakiwa kwenda kwa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh), basi ni mpotofu, mwenye kwenda kinyume na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na maafikiano ya waislamu.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 232-233
- Imechapishwa: 27/04/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)