156 – Tunawachukia wale wanaowachukia na kuwataja kwa njia isiyokuwa nzuri. Hatuwataji isipokuwa tu kwa njia nzuri.

157 – Kuwapenda ni dini, imani na wema.

158 – Kuwachukia ni ukafiri, unafiki na kuchupa mipaka.

MAELEZO

Ambaye anawachukia Maswahabah anaichukia dini, kwa sababu wao ndio waliofikisha Uislamu na wafuasi wa Mteule (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hivyo yule mwenye kuwachukia amechukia Uislamu. Hilo linafahamisha kuwa ndani ya nyoyo za watu hawa hakuna imani na kwamba hawaupendi Uislamu.

Haijuzu kuingilia ile mizozo iliotokea kati yao, kutokana na tulivyotangulia kusema. Bali ni lazima kujizuilia kutokana na hilo na wala wasitajwe isipokuwa tu kwa njia nzuri. Maswahabah. Kuwapenda na kuwakadiria Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) ni moja katika misingi mikuu ambayo muislamu anatakiwa kuitambua. Hilo ni katika imani. Sambamba na hilo kuwachukia, au kumchukia yeyote katika wao, ni katika ukafiri na unafiki. Jengine ni kwa sababu kuwapenda ni katika kumpenda Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), na kuwachukia ni katika kumchukia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 232
  • Imechapishwa: 27/04/2025