Tambua ya kwamba inapendekezwa kuleta Takbiyr baada ya swalah ya Fajr ya siku ya ´Arafah hadi mwisho wa siku za Tashriyq. Takbiyr inasemwa hivi:

الله أكبر ، الله أكبر ، لا إله إلا الله ، والله أكبر ، الله أكبر ولله الحمد

”Allaah ni Mkubwa, Allaah ni Mkubwa, Allaah ni Mkubwa, Allaah ni Mkubwa, Allaah ni Mkubwa na himdi zote njema ni za Allaah.”

Imepokewa kwamba kulisemwa kuambiwa Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah): “Kwa Hadiyth ipi unategemea kuwa Takbiyr huanza baada ya swalah ya Fajr ya siku ya ´Arafah hadi mwisho wa siku za Tashriyq?” Akajibu: “Kwa maafikiano ya ´Umar, ´Aliy, Ibn ´Abbaas na Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhum).”[1]

´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleeza:

“Tulirauka pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutoka Minaa kuelekea ´Arafah, baadhi yetu wakileta Talbiyah na wengine wakileta Takbiyr.”[2]

Ameipokea Muslim.

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea mfano wake kutoka kwa Anas[3].

Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Maoni sahihi zaidi kuhusu Takbiyr ni ile iliyokubaliwa na wengi wa Maswahabah na maimamu, nayo ni kuwa Takbiyr inaletwa kuanzia swalah ya Fajr ya siku ya ´Arafah hadi mwisho wa siku za Tashriyq, baada ya kila swalah.”[4]

[1] al-Mughniy (3/289), ”al-Majmuu´” cha an-Nawawiy (5/35), ”Irwaa’-ul-Ghaliyl” (3/125).

[2] Muslim (1284).

[3] al-Bukhaariy (3/510 Fath) na Muslim (1284).

[4] Majmuu´-ul-Fataawaa (24/220-222).

  • Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 34-35
  • Imechapishwa: 14/05/2025