21. Radd juu ya utata wa Tawassul zao za kizushi na zilizoharamishwa

8 – Miongoni mwa shubuha zao ni pale wanapotumia dalili maneno Yake (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ

“Enyi walioamini! Mcheni Allaah na tafuteni njia za kumkurubia.”[1]

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ

“Hao wanaowaomba [wao wenyewe] wanatafuta kwa Mola wao njia [na] kumkurubia kadri wanavyoweza… ”

Wamefahamua kupitia Aayah hizo kwamba Shari´ah inakubali kuchukua mkati na kati baina yao na Allaah katika Mitume na waja wema kwa njia ya kwamba wanafanya Tawassul kwa dhati, haki na jaha zao.

Jibu ni kwamba wasiylah iliyotajwa katika Aayah mbili sio kama walivofahamu wao. Bali makusudio yake ni kujikurubisha kwa Allaah kwa kufanya matendo mema.

[1] 05:35

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Haqiyqat-it-Tawhiyd, uk. 37
  • Imechapishwa: 01/04/2019