Allaah amemlaani katika Qur-aan yule mwenye kueneza ufisadi katika ardhi, akawakata ndugu zake na akamuudhi Yeye na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Amemlaani yule mwenye kuficha yale aliyoteremsha Allaah katika yale yenye kuweka wazi na uongofu.

Amemlaani yule mwenye kuwatuhumu machafu waumini wanawake ambao wametakasika na ni wenye kujilinda na machafu.

Amemlaani yule mwenye kuonelea kuwa dini ya makafiri ni ongofu zaidi kuliko ya waumini.

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemlaani mwanaume mwenye kuvaa mavazi ya mwanamke na mwanamke mwenye kuvaa mavazi ya mwanaume.

Amewalaani vilevile watenda madhambi wengine.

Lau kungelikuwa hakuna madhara mengine zaidi ya kwamba mtenda dhambi anapatwa na laana ya Allaah, Mtume na Malaika, basi ingelitosheleza kwake kuacha madhambi.

  • Mhusika: Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Daa’ wad-Dawaa’, uk. 74-75
  • Imechapishwa: 09/01/2018