Kwa haya tunajibu kuhusu zile Hadiyth tunazosema ni Swahiyh ambazo hazikutolewa na Imaam al-Bukhaariy. Kwa sababu al-Bukhaariy alipokea tu yale yaliyo Swahiyh kwa upande wa cheni, wala hakupokea kila kilicho Swahiyh kwa ujumla. Ndiyo maana al-Bukhaariy amesema kwamba hakuingiza katika kitabu cha ”al-Jaami´” isipokuwa kilicho Swahiyh na akaacha baadhi ya Swahiyh kwa sababu ya urefu. Muslim pia alisema kwamba si kila kitu kilicho Swahiyh kwake amekipokea hapa, bali ameweka yale waliyokubaliana juu yake. Ndiyo maana an-Nawawiy amesema:
”Hawakukusanya Swahiyh yote wala hawakulazimisha kufanya hivyo.”[1]
Dhahiri ya maneno yao inaonyesha kwamba waliacha pia baadhi ya yaliyokuwa Swahiyh kwa upande wa cheni, ambao ndio mwelekeo wa wanazuoni wa Hadiyth, kwa kukhofia urefu. Basi ni kwa kipaumbele zaidi kwamba waliacha yale yaliyo Swahiyh kwa upande usio wa cheni, nayo ndiyo Swahiyh kwa sababu ya dalili nyingine. Hilo ni kwa sababu Swahiyh kwa sababu ya dalili nyingine haina kanuni inayoendelea kwa mtiririko mmoja, bali ni jambo analolitambua mwenye msimamo thabiti katika misingi na matawi, mwenye juhudi kubwa katika kusoma uongofu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), mwenye maarifa ya siri ya Shari´ah na kufahamu kiini cha Fiqh katika dini. Baadhi ya wanazuoni wachunguzi walikuwa wakiita njia hii kuwa ni njia ya kukubali masimulizi kwa dalili ili kulinganisha na kile walichokijadili wanazuoni wa misingi katika suala la kurejesha masimulizi kwa dalili, kama utakavyoona imefafanuliwa katika ”al-Musawwadah” na katika vitabu vingine virefu vya misingi. Kauli ya ”al-Musawwadah” ni ”miongoni mwa mambo yanayopendeleza masimulizi na kuipa kipaumbele ni kuungwa mkono na ujumla wa Qur-aan, Sunnah, kipimo au maana ya kiakili”. Wanazuoni wengi wa misingi wameona kwamba Hadiyth inayopokelewa kwa kukubaliwa inafidisha elimu. Vivyo hivyo ile Hadiyth iliyopewa nguvu na matendo ya Maswahabah, na pia yale waliyokhitilafiana baina ya wenye kuikubali na wengine wakaifasiri, na ile inayoafikiana na Aayah ya Qur-aan, kanuni na msingi miongoni mwa misingi ya dini na maarifa au inayoafikiana na jambo lililowekwa Kishari´ah kwa mlingano unaosahihisha mfanano baina yao.
Ikiwa haya yamebainika, basi Hadiyth ya soksi ni miongoni mwa Hadiyth zilizopokelewa kwa kukubaliwa[2], imeungwa mkono na matendo ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) na imeenda sambamba na kisomo:
وَأَرْجُلِكُمْ
”… na miguu yenu…”
na:
وَأَرْجُلَكُمْ
”… na miguu yenu… ”
na inaingia chini ya kanuni ya kuondoa uzito na inaenda sambamba na kupangusa juu ya soksi za ngozi. Mambo haya yote ni miongoni mwa yanayosahihisha masimulizi kwa usahihishaji mkubwa kabisa. Kwa ujumla zimekusanyika katika Hadiyth ya soksi aina mbili za usahihi kwa pamoja:
1 – Usahihi wake kwa upande wa cheni kwa mujibu wa at-Tirmidhiy na Ibn Hibbaan, kama tulivyothibitisha kwa kuondoa dai la hali isiyo ya kawaida lililodaiwa ndani yake.
2 – Usahihi wake kwa upande usio wa cheni, jambo ambalo nimelitaja sasa hivi. Pindi Hadiyth inaposihi, basi hapana chochote isipokuwa kusikia na kutii.
[1] Tadriyb-ur-Raawiy, uk. 28.
[2] Tayari umefahamu kutokana na yaliyotangulia kwamba Hadiyth inayopokelewa kwa kukubaliwa haiwi Swahiyh isipokuwa kwa masharti mawili. Sharti la kwanza ni kwamba ienee na kujulikana miongoni mwa maimamu wa Hadiyth bila kukataliwa na yeyote miongoni mwao. Hadiyth hii, japokuwa cheni yake ni Swahiyh kwetu sisi, imekataliwa na baadhi ya waliokwishakutajwa katika maneno ya mwandishi na ya Shaykh Ahmad Shaakir. Basi katika hali hiyo sioni ifae kusemwa kwamba ni miongoni mwa Hadiyth zilizopokelewa kwa kukubaliwa. Bali miongoni mwao wapo walioikubali na miongoni mwao wapo walioirudisha. Haki iko pamoja na wa kwanza bila shaka. Hoja ni cheni yake thabiti. Naam, inaungwa mkono na inaongezewa nguvu zaidi na kuendelea kwa matendo ya Swahabah juu yake, kama itakavyokuja baadaye.
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 38-40
- Imechapishwa: 08/04/2026

Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 38-40
Imechapishwa: 08/04/2026
https://firqatunnajia.com/21-hakuna-jengine-isipokuwa-kisikiliza-na-kutii/