21. Epuka kutia wanja na kupalizia na kusukutua kwa kishindo

Mfungaji anatakiwa kuepuka kutia wanja macho au kutia dawa kwenye macho kwa zile dawa za matone au nyenginezo katika kipindi cha funga kwa ajili ya kuilinda swawm yake.

Asifanye kishindo wakati wa kusukutua na kupalizia. Kwani kwa kufanya hivo pengine maji yakaingia tumboni mwake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Fanya kishindo katika kupalizia isipokuwa kama utakuwa umefunga.”[1]

[1] Abu Daawuud (142), at-Tirmdihiy (787), an-Nasaa´iy (87) na Ibn Maajah (407).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/384)
  • Imechapishwa: 05/04/2021