Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
153 – Allaah anaghadhibika na kuridhia, si kama yeyote katika viumbe.
MAELEZO
Miongoni mwa sifa za Allaah (´Azza wa Jall) za kimatendo ni kuwa anaghadhibika na kuridhia. Allaah (Subhaanah) amesema:
وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ
“Wale waliotangulia mwanzoni ambao ni Muhaajiruun na Answaar na wale waliowafuata kwa wema, Allaah ameridhika nao nao wameridhika Naye.”[1]
Allaah huwaridhia waja Wake:
وَرِضْوَانٌ مِّنَ اللَّـهِ أَكْبَرُ
”… na radhi kutoka kwa Allaah ndio kubwa zaidi.”[2]
لَّقَدْ رَضِيَ اللَّـهُ عَنِ الْمُؤْمِنِينَ إِذْ يُبَايِعُونَكَ تَحْتَ الشَّجَرَةِ
”Hakika Allaah amewawia radhi waumini waliokupa kiapo cha usikivu na utiifu chini ya mti.”[3]
Vilevile hughadhibika (Subhaanahu wa Ta´ala):
قُلْ هَلْ أُنَبِّئُكُم بِشَرٍّ مِّن ذَٰلِكَ مَثُوبَةً عِندَ اللَّـهِ ۚ مَن لَّعَنَهُ اللَّـهُ وَغَضِبَ عَلَيْهِ
”Sema: “Je, nikujulisheni yule ambaye ni mwenye malipo mabaya zaidi kuliko haya mbele ya Allaah? Yule ambaye Allaah amemlaani na akamghadhibikia.”[4]
Allaah anamghadhibikia na kumchukia anayemuasi. Amesema (Ta´ala):
وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا
“Na yeyote atakayemuua muumini makusudi, basi malipo yake ni Moto ni mwenye kudumishwa humo na Allaah atamghadhibikia na atamlaani na atamuandalia adhabu kuu.”[5]
Kiumbe naye hughadhibika na kuridhia. Hata hivyo hakufanani kati ya kughadhibika na kuridhia kwa kiumbe na kughadhibika na kuridhia kwa Muumba. Kuridhia na kughadhibika kwa Allaah kunalingana Naye (Subhaanah), na kuridhia na kughadhibika kwa kiumbe kunalingana naye. Vivyo hivyo kuhusiana na sifa zingine zote:
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖوَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.”[6]
Hakuna anayefanana Naye katika dhati, majina wala sifa Zake. Ingawa Yeye na viumbe wako na majina na sifa, hazifanani.
[1]9:100
[2]9:72
[3]48:18
[4]5:60
[5]4:93
[6]42:11
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 223-224
- Imechapishwa: 21/04/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)