Zaidi ya hayo lau tungetaka kushindana kwa wingi wa wanaoidhoofisha, basi tungeshindana naye kwa kumtajia wengi zaidi. Kwa sababu kupangusa juu ya soksi kumepokelewa kutoka kwa Maswahabah, akiwemo ´Umar bin al-Khattwaab, ´Aliy, Abu Mas´uud, al-Baraa´, Anas, Abu Umaamah, Sahl, ´Amr bin Hurayth, Ibn ´Abbaas, Ibn ´Umar, Ibn Abiy Waqqaas, ´Ammaar, Bilaal, Ibn Abiy Awfaa, al-Mughiyrah na Abu Muusa (Radhiya Allaahu ´anhum).
Miongoni mwa wanafunzi wa Maswahabah ni pamoja na Qataadah, Ibn al-Musayyib, Ibn Jurayj, ´Atwaa, an-Nakha´iy, al-Hasan, Khilaasw, Ibn Jubayr na Naafiy´ (Rahimahum Allaah). Cheni za wapokezi kufika mpaka kwao ni jambo litakuja huko mbele. Hapana shaka yoyote kwamba kitendo cha mabwana hawa wakubwa cha kuifanyia kazi ni miongoni mwa mambo yanayoiunga mkono kusihi kwa Hadiyth ya al-Mughiyrah, kuitia nguvu na kuisahihisha. Kwa sababu ikiwa hawakufanya hivo kwa kutegemea kusihi kwa cheni yake, basi wamefanya hivo kutokana na cheni nyingine ya wapokezi iliyo katika maana yake. Hakuna mtu mwenye uelewa japo mdogo anayeweza kutilia shaka jambo hilo. Zaidi ya hayo Hadiyth ya kupangusa juu ya soksi imepokelewa kwa kuikubali Abu Haniyfah, ash-Shaafi´iy, Ahmad bin Hanbal, Ishaaq, Daawuud adh-Dhwaahiriy na Ibn Hazm. Hawa wote ni maimamu wa Fiqh na ijtihadi. Wote wameijengea hoja katika Fiqh iliyonukuliwa kutoka kwao. Ni jambo linalotambulika katika elimu ya istilahi ya Hadiyth[1] kwamba Hadiyth huhukumiwa kuwa Swahiyh ikiwa watu wameipokea kwa kuikubali[2], hata kama haina cheni Swahiyh[3]. Abul-Hasan Ibn al-Hasswaar amesema katika ”Taqriyb-ul-Madaarik ´alaa Muwattwa’ Maalik”:
”Mwanachuoni anaweza kujua usahihi wa Hadiyth ikiwa katika cheni yake hakuna mwongo, kwa kulingana kwake na Aayah ya Qur-aan au baadhi ya misingi ya Shari´ah, jambo hilo likamfanya kuikubali na kuitendea kazi.”
Hii huitwa Swahiyh kupitia zingine. Hadiyth ambayo ni Swahiyh kupitia zingine ni sawa na Swahiyh kwa dhati yake inapokuja katika kuijengea hoja, kufanyia kazi muqtadha yake na kufanyia kazi ujumla wake, upekee wake, yale yaliyoachiwa na yale yaliyofungamanishwa. Kama alivyobainisha Ibn-ul-Hasswaar, mwanachuoni ambaye uwezo wa kufanya ijtihadi, anaweza kujua usahihi wa Hadiyth kwa upande usio wa cheni.
[1] Tadriyb-ur-Raawiy, uk. 15.
[2] Watu katika mtiririko hapa kunakusudiwa wanazuoni katika Hadiyth. Kwa maana kwamba kuna Hadiyth nyingi ambazo zimepokelewa kwa kukubaliwa na wanazuoni wa Fiqh au watu wengine ilihali ni dhaifu, zinazokwenda kinyume na zenye kukataliwa kwa wanazuoni wa Hadiyth! Moja katika Hadiyth hizo ni ile Hadiyth ya Mu´aadh kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia:
”Utahukumu kwa nini?” Akasema: ”Kwa Kitabu cha Allaah.” Akasema: ”Ikiwa hukupata?” Akasema: ”Kwa Sunnah ya Mtume wa Allaah… ”
Kama alivyosema imamu wa maimamu al-Bukhaariy (Rahimahu Allaah) ni kwamba Hadiyth hii ni dhaifu na yenye kupingana. Nimeitaja katika “Silsilat-ul-Ahaadiyth adh-Dhwa´iyfah”.
Kisha haitoshi kusema kwamba ni wanazuoni wa Hadiyth – bali lazima iongezwe sharti jingine, nalo ni kukubaliana kwao juu yake. Hilo limeashiriwa na as-Suyuutwiy alipomnukuu al-Isfaraayiyniy, ambaye amesema:
“Usahihi wa Hadiyth hutambuliwa pale inapojulikana na kuenea kwa maimamu wa Hadiyth bila kukataliwa na yeyote miongoni mwao.” (Tadriyb-ur-Raawiy (1/67))
[3] Maana yake ni kwamba lazima iwe na cheni fulani. Hata hivyo hairuhusiwi iwe dhaifu sana, kama yanavyoashiri maneno ya Abul-Hasan Ibn al-Hasswaar yatakayokuja katika kitabu. Hadiyth inayopokelewa kwa kukubaliwa haiwi Swahiyh isipokuwa ikiwa ina cheni inayofaa kuzingatiwa. Nayo ndiyo inayopata nguvu kwa kukubaliwa huko. Lihifadhi hili, kwani ni jambo muhimu sana.
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 37-39
- Imechapishwa: 07/04/2026

Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 37-39
Imechapishwa: 07/04/2026
https://firqatunnajia.com/20-salaf-waliofuta-juu-ya-soksi/