Wale wa mwanzo wanagawanyika katika makundi mawili. Wakati mwingine wanayapokonya maana ya matamshi ya Qur-aan na makusudio yake halisi, na mara nyingine wanayafasiri kwa maana ambayo haikutajwa wala haikukusudiwa. Katika hali zote mbili mara nyingine inawezekana kile wanachotaka kukikanusha au kuthibitisha ni batili, hivyo kosa lao linakuwa katika dalili na kile kinachotolewa dalili. Mara nyingine kinaweza kuwa ni haki, hivyo kosa lao linakuwa katika dalili na si kile kinachotolewa dalili. Hali hii kama ilivyotokea katika tafsiri ya Qur-aan pia imetokea katika tafsiri ya Hadiyth.
Wale waliokosea katika dalili na kile kinachotolewa dalili, ni kama yale yanayofanywa na baadhi ya makundi ya Ahl-ul-Bid´ah ambao wanagawanya I´tiqaad zinazoenda kinyume na haki ambayo ummah bora – kama zile karne bora za kwanza na maimamu wake – uko juu yake na ambao hawakusanyiki juu ya upotofu, baada ya hapo wanajaribu kuielekea Qur-aan na kuifasiri kwa mujibu wa maono yao wenyewe, wakati fulani wanazitumia Aayah kama ushahidi wa maono yao hata hivyo Aayah hizo hazina dalili yoyote ya kuunga mkono na wakati mwingine wanayafasiri yale mambo yanayopingana na ´Aqiydah zao na kuyapotosha maneno kutoka mahali pake stahiki. Miongoni mwa watu hao ni Khaawarij, Raafidhwah, Jahmiyyah, Mu’tazilah, Qadariyyah na Murji-ah.
- Muhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Muqaddimah fiy Usuwl-it-Tafsiyr, uk. 73
- Imechapishwa: 03/04/2025
Wale wa mwanzo wanagawanyika katika makundi mawili. Wakati mwingine wanayapokonya maana ya matamshi ya Qur-aan na makusudio yake halisi, na mara nyingine wanayafasiri kwa maana ambayo haikutajwa wala haikukusudiwa. Katika hali zote mbili mara nyingine inawezekana kile wanachotaka kukikanusha au kuthibitisha ni batili, hivyo kosa lao linakuwa katika dalili na kile kinachotolewa dalili. Mara nyingine kinaweza kuwa ni haki, hivyo kosa lao linakuwa katika dalili na si kile kinachotolewa dalili. Hali hii kama ilivyotokea katika tafsiri ya Qur-aan pia imetokea katika tafsiri ya Hadiyth.
Wale waliokosea katika dalili na kile kinachotolewa dalili, ni kama yale yanayofanywa na baadhi ya makundi ya Ahl-ul-Bid´ah ambao wanagawanya I´tiqaad zinazoenda kinyume na haki ambayo ummah bora – kama zile karne bora za kwanza na maimamu wake – uko juu yake na ambao hawakusanyiki juu ya upotofu, baada ya hapo wanajaribu kuielekea Qur-aan na kuifasiri kwa mujibu wa maono yao wenyewe, wakati fulani wanazitumia Aayah kama ushahidi wa maono yao hata hivyo Aayah hizo hazina dalili yoyote ya kuunga mkono na wakati mwingine wanayafasiri yale mambo yanayopingana na ´Aqiydah zao na kuyapotosha maneno kutoka mahali pake stahiki. Miongoni mwa watu hao ni Khaawarij, Raafidhwah, Jahmiyyah, Mu’tazilah, Qadariyyah na Murji-ah.
Muhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Muqaddimah fiy Usuwl-it-Tafsiyr, uk. 73
Imechapishwa: 03/04/2025
https://firqatunnajia.com/20-njia-ya-wazushi-ya-kutafsiri-qur-aan/