20. Ni yapi maoni yenu juu ya uongozi?

Swali 20: Ni yapi maoni yenu juu ya uongozi?

Jibu: Tunaitakidi kuwa uteuzi wa kiongozi ni faradhi kwa baadhi ya waislamu.

Ummah hauwezi kuwa pasi na kiongozi ambaye anautekelezea mambo ya dini na ya dunia, kuulinda na mashambulizi ya washambulizi na kuwasimamishia adhabu wahalifu.

Uongozi hautimii isipokuwa kwa kuwepo utiifu katika wema na si katika maasi. Jihaad ni yenye kuendelea na kila kiongozi mwema na mtenda madhambi. Wanatakiwa kusaidiwa katika ya kheri na kunasihiwa katika ya shari.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com