20. Masimulizi ya Maalik kwa mujibu wa Ayyuub bin Swaalih al-Makhzuumiy

8 – Upokezi wa Ayyuub bin Swaalih al-Makhzuumiy[1]

Haafidhw Ibn ´Abdil-Barr (Rahimahu Allaah) amesema: Muhammad bin ´Abdil-Malik[2] ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Yuunus[3] ametuhadithia: Baqiyy bin Makhlad[4] ametuhadithia: Bakkaar bin ´Abdillaah al-Qurashiy[5] ametuhadithia… Akataja yale masimulizi yaliyotangulia kutoka kwa Mahdiy bin Ja’far kisha akasema: Baqiyy amesema: Ayyuub bin Swalaah[6] al-Makhzuumiy ametuhadithia huko Ramlah:

“Tulikuwa kwa Maalik alipojiliwa na muiraki mmoja na kumwambia: “Ee, Abu ´Abdillaah, kuna jambo nataka kukuuliza.” Maalik akainamisha kichwa chake ambapo akamwambia: “Ee Abu ´Abdillaah!

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[7]

Amelingana juu vipi?” Akasema: ”Umeuliza juu ya kitu ambacho si kwamba hakitambuliki na umezungumzia kisichofahamika. Hakika wewe ni mtu muovu. Mtoeni nje!” Wakamshika mkono na kumwondoa nje.”[8]

[1] Ayyuub bin Swaalih bin Salamah al-Haraaniy al-Makhzuumiy al-Madaniy Abu Sulaymaan. Aliishi Ramlah. Amesimulia “al-Muwattwa’” kutoka kwa Maalik. Amedhoofishwa na Ibn Ma’iyn. Ibn ´Adiy amesema:

“Amepwekeka katika kupokea mambo kadhaa kutoka kwa Maalik.”

Tazama “Lisaan-ul-Miyzaan” (1/483), “adh-Dhwu´afaa’ wal-Matruukiyn” (1/131) ya Ibn-ul-Jawziy na “al-Mughniy fiydh-Dhwu’afaa’” (1. /155).

[2] Abu ´Abdillaah Muhammad bin ´Abdil-Malik bin Dhwayfuun al-Lakhmiy al-Qurtwubiy al-Haddaad. Ibn-ul-Faradhwiy amesema juu yake:

“Alikuwa mtu mwema na mmoja katika waadilifu. Watu wameandika juu yake. Baada ya muda alichanganya mambo ambayo alikuwa alisomewa. Hakuwa miongoni mwa watu waliosikia wala katika watu wenye kudhibiti.”

Alikufa mnamo 492.

Tazama “Taariykh-ul-‘Ulamaa’” (2/100) cha Ibn-ul-Faradhwiy, “Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (17/56) na “Lisaan-ul-Miyzaan” (5/267 ) na Ibn Hajar. Katika “Lisaan-ul-Miyzaan” kumejitokeza kosa la uchapishaji kwamba ni Muhammad bin ´Abdil-Malik bin Swafwaan.

[3] Abu Muhammad ´Abdullaah bin Yuunus bin Muhammad bin ´Ubaydillaah al-Muraadiy, anayejulikana kama al-Qabriy kutoka Andalusia. Alikuwa ni swahiba wa Baqiyy bin Makhlad ambaye amesikia “al-Muswannaf” ya Ibn Abiy Shaybah. Alikufa mnamo 330.

Tazama “Taariykh-ul-´Ulamaa’” (1/265) cha Ibn-ul-Faradhwiy na “Tawdhwiyh-ul-Mushtabih” (7/178) cha Ibn Naaswir-id-Diyn.

[4] Abu ´Abdir-Rahmaan Baqiyy bin Makhlad bin Yaziyd al-Andalusiy al-Qurtwubiy. Ibn-ul-Faradhwiy amesema:

“Baqiy alikuwa mchamungu, mwema na mwenye kuipa nyongo dunia.”

adh-Dhahabiy amesema juu yake:

“Imaam, mwennye kuigiliza na Shaykh-ul-Islaam… Alikuwa mwenye kuhifadhi ambaye alikuwa akifasiri na kusimulia cheni mbili zisizo na kifani.”

Alikufa mnamo 276.

Tazama “Taariykh-ul-‘Ulamaa’” (1/107-109) na “Siyar A´laam-in-Nubalaa’” (13/285).

[5] Bakkaar bin ´Abdillaah bin Busr ad-Dimashqiy al-Qurashiy. Abu Haatim amesema juu yake:

“Ni mkweli.” (al-Jarh wat-Ta´diyl (2/410))

[6] Imekuja namna hii katika ”at-Tamhiyd”, ni kosa.

[7] 20:05

[8] at-Tamhiyd (7/151).

  • Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 37-39
  • Imechapishwa: 29/11/2025