135 – Khalaf bin Hishaam ametuhadithia: Hammaad bin Zayd ametuhadithia, kutoka kwa Shu´ayb bin al-Habhaab, kutoka kwa Abu Sa´iyd, ambaye amesema:
”Niliingia kwa ´Aaishah na nikamuona anashona nguo yake. Nikamwambia: ”Ee Mama wa waumini! Je, Allaah (´Azza wa Jall) hakukupanua riziki?” Akasema: ”Hakuna jipya kwa yule asiyekivaa cha zamani.”
136 – Muhammad bin Muusa al-Harashiy ametuhadithia: Ja´far bin Sulaymaan ametuhadithia, kutoka kwa Maalik bin Diynaar: Mzee mmoja amenihadithia, kutoka kwa al-Hasan, ambaye amesema:
”Abu Muusa alimuozesha mmoja wa wanawe na akafanya karamu ya ndoa kwa ajili yake, akawaalika watu. Tukiwa ndani ya nyumba ikasemwa kwamba amekuja kiongozi wa Waumini. ´Aliy bin Abiy Twaalib akaingia na watu wengine akiwa na fimbo mkononi na amevaa kanzu isiyo na mifuko.”
137 – Daawuud bin Rushayd ametuhadithia: ´Aliy bin Haashim ametuhadithia, kutoka kwa adh-Dhwahhaak bin ´Umayrah, ambaye amesema:
”Niliona kanzu ya ´Aliy aliyouliwa nayo ambayo ilikuwa imetengenezwa kwa pamba ngumu. Niliona alama ya damu yake ndani yake kama rangi ya madini mekundu.”
138 – Kwa njia hiyohiyo ametuhadithia Ismaa´iyl al-Bazzaar, kutoka kwa Umm Muusa, ambaye alikuwa mfanya kazi wa ´Aliy, ambaye amesema:
”Sijawahi kumuona ´Aliy amevaa kanzu laini zaidi kuliko Duurmaaniy.” Nikasema: ”Alikuwa akivaa nini?” Akasema: ”Pamba ngumu.”
139 – Surayj ametuhadithia: Hushaym ametuhadithia, kutoka kwa Ismaa´iyl bin Saalim, kutoka kwa Abu Idriys, ambaye amesema:
”´Aliy alienda sokoni akasema: ”Nani ana kanzu nzuri kwa dirhamu tatu?” Mtu mmoja akasema: ”Mimi ninayo.” Akasema: ”Ilete.” Akaleta, ikampendeza. ´Aliy akasema: ”Bei yake ni zaidi ya hii?” Akasema: ”Hapana.” Akasema: ”Nikamuona akifungua fundo la mkono wa kanzu, ndani yake kulikuwa na pesa alizohifadhi, akavaa, ikawa inazidi kwenye ncha za vidole vyake, akasema: ”Kateni kinachozidi kwenye ncha za vidole vyangu kisha ishone.”
140 – Surayj amenihadithia: Muhammad bin Rabiy´ah ametuhadithia, kutoka kwa Mudrik bin Shawdhab, ambaye amesema:
”Nilimuona ´Aliy mkono wake wa kanzu umeishia kwenye kifundo cha mkono.”
141 – Khalaf bin Saalim ametuhadithia: Abu Nu´aym ametuhadithia: Shurayk ametuhadithia, kutoka kwa ´Uthmaan ath-Thaqafiy, kutoka kwa Zayd bin Wahb, aliyesema:
”´Aliy alikosolewa kuhusu vazi lake ambapo akasema: ”Hakika vazi langu hili ni mbali zaidi na kiburi na linafaa zaidi kuigwa na muislamu.”
142 – ´Abdur-Rahmaan bin Swaalih amenihadithia: Yuunus bin Bukayr ametuhadithia, kutoka kwa ´Anbasah bin al-Azhar, kutoka kwa Yahyaa bin ´Uqayl, ambaye amesema:
´Aliy bin Abiy Twaalib alimwambia ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa): “Ukitaka kuungana na marafiki zako wawili, basi punguza matarajio, kula bila ya kushiba, kunja nguo yako ya chini na tengeneza viatu – basi utaungana nao.”
- Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 177-184
- Imechapishwa: 04/02/2026

Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 177-184
Imechapishwa: 04/02/2026
https://firqatunnajia.com/20-kama-unataka-kuungana-na-mtume-na-abu-bakr/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket