Baadhi ya Salaf wamesema:
“Ewe mwana wa Aadam! Wewe ni mwenye haja zaidi kwa fungu lako la Aakhirah kuliko dunia. Ukianza na fungu lako la dunia, utapoteza sehemu yako ya Aakhirah na utakuwa ndani ya dunia katika khatari. Lakini ukianza na fungu lako la Aakhirah, basi utapata pia fungu lako la dunia na utaiweka kwa mpangilio mzuri.”
´Umar bin ´Abdil-´Aziyz (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa akisema katika Khutbah zake:
“Enyi watu! Hakika hamkuumbwa bure na wala hamkuachwa kiholela. Hakika mna mahali pa kurejea ambapo Allaah (´Azza wa Jall) atawakusanya kwa ajili ya kutoa hukumu kati yenu na kuhukumu baina yenu. Basi amepata khasara na ni mwenye mashaka yule ambaye Allaah atamtoa katika rahmah Yake ambayo imekienea kila kitu na kutoka katika Pepo Yake ambayo upana wake ni kama wa mbingu na ardhi. Hakika si vyenginevyo salama Kesho ni kwa yule aliyemwogopa Allaah (Ta´ala) na akamcha, akauza kidogo kwa kingi, kilicho fanaa kwa cha kudumu na mashaka kwa furaha. Je, hamuoni kwamba nyinyi mpo katika migongo ya waliokwishakufa na baada yenu watawarithi waliobakia? Je, hamuoni kwamba kila siku mnasindikiza asubuhi na jioni mtu anayerejea kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), ambaye muda wake umekwishamalizika, matumaini yake yamekatika na mnamuweka ndani ya shimo la ardhi lenye ufa, bila mto wala godoro, ameacha sababu zote na kuagana na wapenzi na anakutana na hesabu?”[1]
Makusudio ni kwamba Allaah (´Azza wa Jall) amempa mja katika muda huu mfupi jeshi, vifaa na misaada. Aidha akamueleza kwa nini ataweza kujilinda na adui yake na ni kwa nini anaweza kuikomboa nafsi yake anapotekwa.
[1] Hilyat-ul-Awliyaa’ (5/266, 287 na 295).
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 33-37
- Imechapishwa: 04/08/2025
Baadhi ya Salaf wamesema:
“Ewe mwana wa Aadam! Wewe ni mwenye haja zaidi kwa fungu lako la Aakhirah kuliko dunia. Ukianza na fungu lako la dunia, utapoteza sehemu yako ya Aakhirah na utakuwa ndani ya dunia katika khatari. Lakini ukianza na fungu lako la Aakhirah, basi utapata pia fungu lako la dunia na utaiweka kwa mpangilio mzuri.”
´Umar bin ´Abdil-´Aziyz (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa akisema katika Khutbah zake:
“Enyi watu! Hakika hamkuumbwa bure na wala hamkuachwa kiholela. Hakika mna mahali pa kurejea ambapo Allaah (´Azza wa Jall) atawakusanya kwa ajili ya kutoa hukumu kati yenu na kuhukumu baina yenu. Basi amepata khasara na ni mwenye mashaka yule ambaye Allaah atamtoa katika rahmah Yake ambayo imekienea kila kitu na kutoka katika Pepo Yake ambayo upana wake ni kama wa mbingu na ardhi. Hakika si vyenginevyo salama Kesho ni kwa yule aliyemwogopa Allaah (Ta´ala) na akamcha, akauza kidogo kwa kingi, kilicho fanaa kwa cha kudumu na mashaka kwa furaha. Je, hamuoni kwamba nyinyi mpo katika migongo ya waliokwishakufa na baada yenu watawarithi waliobakia? Je, hamuoni kwamba kila siku mnasindikiza asubuhi na jioni mtu anayerejea kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), ambaye muda wake umekwishamalizika, matumaini yake yamekatika na mnamuweka ndani ya shimo la ardhi lenye ufa, bila mto wala godoro, ameacha sababu zote na kuagana na wapenzi na anakutana na hesabu?”[1]
Makusudio ni kwamba Allaah (´Azza wa Jall) amempa mja katika muda huu mfupi jeshi, vifaa na misaada. Aidha akamueleza kwa nini ataweza kujilinda na adui yake na ni kwa nini anaweza kuikomboa nafsi yake anapotekwa.
[1] Hilyat-ul-Awliyaa’ (5/266, 287 na 295).
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 33-37
Imechapishwa: 04/08/2025
https://firqatunnajia.com/20-huyu-pekee-ndiye-aliye-salama/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket