20. Haya ndio madhambi yanayofutwa na swawm ya ´Arafah

Ikiwa siku ya ´Arafah itaangukia siku ya ijumaa bado inafaa kufunga. Ama kuhusu katazo la kufunga ijumaa peke yake, hilo linahusu mtu kufunga ijumaa kwa ajili ni siku ya ijumaa. Lakini siku ya ´Arafah inafungwa kwa sababu ya nafasi yake ya kipekee, ni mamoja iwe ni ijumaa au siyo. Hii inafahamisha kuwa ijumaa siyo lengo, bali ni ´Arafah.

Madhambi yanayofutwa kwa kufunga siku ya ´Arafah ni yale madogo. Kuhusu madhambi makubwa kama uzinifu, kula ribaa, uchawi na mfano wake, haya hayafutwi na matendo mema pekee. Bali ni lazima mtu atubie ya kweli au utekelezaji wa adhabu kama ipo. Haya ndio maoni ya kikosi kikubwa cha wanazuoni.

Muislamu anapaswa kufanya juhudi katika kuomba du´aa siku hiyo kwa kutarajia jawabu, kwa sababu du´aa ya aliyefunga ni yenye kuitikiwa. Akiomba wakati wa kufuturu, basi ni karibu zaidi kujibiwa na kupokelewa.

  • Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 33-34
  • Imechapishwa: 14/05/2025