Abu Daawuud (1/248) amesema: ´Abdul-Wahhaab bin Najdah ametuhadithia: Baqiyyah na Shu´ayb bin Ishaaq ametuhadithia, kutoka kwa al-Awzaa´iy: Muhammad bin al-Waliyd amenihadithia, kutoka kwa Sa´iyd bin Abiy Sa´iyd, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:
”Mmoja wenu akiswali na kuvua viatu vyake, basi asimuudhi mtu yeyote. Aviweke kati ya miguu yake au aswali navyo.”
Ameipokea Ibn Abiy Shaybah (2/418), at-Twabaraaniy katika “as-Swaghiyr” (2/8), al-Haakim, ambaye amesema kuwa “Hadiyth ni Swahiyh kwa za Muslim. Si al-Bukhaariy wala Muslim hakuna aliyeipokea” na al-Bayhaqiy (2/432).
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 20-21
- Imechapishwa: 04/06/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket