Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
145 – Matendo ya viumbe yameumbwa na Allaah na ni machumo ya waja.
MAELEZO
Kuna makinzano juu ya masuala haya ambapo kuna mitazamo tofauti na nadharia potofu: matendo ya waja yameumbwa na Allaah au waja wenyewe?
Maoni ya kwanza watetezi wake ni ya Jabriyyah na Jahmiyyah. Wanasema kuwa mja ametenzwa nguvu na hana chochote kuhusiana na matendo. Matendo si chochote isipokuwa ni uumbaji wa Allaah (´Azza wa Jall). Swalah inayoswaliwa na mtu sio kwa kutaka kwake mwenyewe – ametenzwa nguvu kwayo. Watu hawa wamechupa mipaka katika kuthibitisha uwezo wa Allaah. Nadharia yao ni upotofu wa wazi na hiyo maana yake ni kwamba Allaah anawadhulumu na anawaadhibu kwa mambo ambayo hawana khiyari na hawayawezi. Kwa msemo mwingine Allaah anamuadhibu na kumlipa thawabu mtu kwa kitendo cha mtu mwingine. ´Aqiydah hii ndio mbaya kabisa ukilinganisha na zingine.
Maoni ya pili yanaenda kinyume kabisa na yale ya kwanza na watetezi wake ni Mu´´tazilah. Wanasema kuwa matendo ni uzalishaji wa mja na utashi na matakwa yake ya moja kwa moja. Vilevile wanadai kuwa Allaah hana chochote kuhusiana na matendo yake na kwamba mja ndiye ambaye anaumba matendo yake mwenyewe. Watu hawa wamechupa mipaka katika kuthibitisha matakwa ya mja. ´Aqiydah yao inapelekea kwamba Allaah si mwenye kuweza na kwamba anashirikiana na wengine katika kuumba na kuunda. Hiyo ndio ´Aqiydah walionayo waabudia moto pia. Kwa ajili hiyo Mu´tazilah wameitwa kuwa ni “waabudia moto wa ummah huu”[1]. Kwa sababu waabudia moto wanasema kuwa ulimwengu una waumba wawili; mmumbaji mmoja anaumba kheri na muumba mwingine anaumba shari. Mu´tazilah wamewapiku na kusema kuwa kila mmoja anajiumbia matendo yake mwenyewe. Kwa ajili hiyo wakathibitisha waumbaji wawili.
[1] Abu Daawuud (4691). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (4691).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 209-210
- Imechapishwa: 09/04/2025
Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
145 – Matendo ya viumbe yameumbwa na Allaah na ni machumo ya waja.
MAELEZO
Kuna makinzano juu ya masuala haya ambapo kuna mitazamo tofauti na nadharia potofu: matendo ya waja yameumbwa na Allaah au waja wenyewe?
Maoni ya kwanza watetezi wake ni ya Jabriyyah na Jahmiyyah. Wanasema kuwa mja ametenzwa nguvu na hana chochote kuhusiana na matendo. Matendo si chochote isipokuwa ni uumbaji wa Allaah (´Azza wa Jall). Swalah inayoswaliwa na mtu sio kwa kutaka kwake mwenyewe – ametenzwa nguvu kwayo. Watu hawa wamechupa mipaka katika kuthibitisha uwezo wa Allaah. Nadharia yao ni upotofu wa wazi na hiyo maana yake ni kwamba Allaah anawadhulumu na anawaadhibu kwa mambo ambayo hawana khiyari na hawayawezi. Kwa msemo mwingine Allaah anamuadhibu na kumlipa thawabu mtu kwa kitendo cha mtu mwingine. ´Aqiydah hii ndio mbaya kabisa ukilinganisha na zingine.
Maoni ya pili yanaenda kinyume kabisa na yale ya kwanza na watetezi wake ni Mu´´tazilah. Wanasema kuwa matendo ni uzalishaji wa mja na utashi na matakwa yake ya moja kwa moja. Vilevile wanadai kuwa Allaah hana chochote kuhusiana na matendo yake na kwamba mja ndiye ambaye anaumba matendo yake mwenyewe. Watu hawa wamechupa mipaka katika kuthibitisha matakwa ya mja. ´Aqiydah yao inapelekea kwamba Allaah si mwenye kuweza na kwamba anashirikiana na wengine katika kuumba na kuunda. Hiyo ndio ´Aqiydah walionayo waabudia moto pia. Kwa ajili hiyo Mu´tazilah wameitwa kuwa ni “waabudia moto wa ummah huu”[1]. Kwa sababu waabudia moto wanasema kuwa ulimwengu una waumba wawili; mmumbaji mmoja anaumba kheri na muumba mwingine anaumba shari. Mu´tazilah wamewapiku na kusema kuwa kila mmoja anajiumbia matendo yake mwenyewe. Kwa ajili hiyo wakathibitisha waumbaji wawili.
[1] Abu Daawuud (4691). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (4691).
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 209-210
Imechapishwa: 09/04/2025
https://firqatunnajia.com/191-misimamo-miwili-potofu-kuhusu-matendo-ya-watu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket