Nilisikia jinsi ambavyo Abu ´Aliy al-Hasan bin Safwaan al-Bardha´iy anavyosomewa katika Rajab mwaka wa 338: Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin ´Ubayd bin Sufyaan bin Abiyd-Dunyaa al-Qurashiy (Rahimahu Allaah) ametuhadithia:

128 – Sa´duuyah ametuhadithia, kutoka kwa ´Abbaad bin al-´Awwaam, kutoka kwa Muhammad bin Ishaaq, kutoka kwa ´Abdullaah bin Abiy Umaamah, kutoka kwa Ka´b bin Maalik, kutoka kwa baba yake, aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Uchakavu ni katika imani.”[1]

129 – Haaruun bin ´Abdillaah ametuhadithia: Ma´n ametuhadithia: ´Abdullaah bin al-Muniyb bin ´Abdillaah bin Abiy Umaamah al-Answaariy, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Mahmuud bin Labiyd, kutoka kwa Abu Umaamah al-Answaariy, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Uchakavu ni katika imani.”

Haaruun amesema:

”Nilimuuliza Ma´n nini maana ya uchakavu. Akasema: ”Ni vazi lililo chini ya ubora wa vazi jingine.”

Akimaanisha vazi la chini.

130 – Yahyaa bin Ayyuub ametuhadithia: ´Aliy bin Haashim ametuhadithia, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Zayd bin Wahb, ambaye ameeleza:

”Nilimuona ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) ametoka kwenda sokoni akiwa na fimbo mkononi mwake na akiwa amevaa kikoi chenye viraka kumi na vinne, ambapo baadhi yake vikiwa vya ngozi.”

131 – Shu´ayb bin Harb ametuhadithia, kutoka kwa Sulaymaan bin al-Mughiyrah, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas, aliyesema:

”Niliona kati ya mabega ya ´Umar (Rahimahu Allaah) viraka vinne.”

132 – Surayj bin Yuunus amenihadithia: ´Aliy bin Haashim ametuhadithia, kutoka kwa Ismaa´iyl al-Bazzaar, kutoka kwa Umm ´Afiyf, ambaye ameeleza:

”Nilimuona ´Aliy bin Abiy Twaalib amevaa shuka nyekundu miongoni mwa mashuka ya wabebaji mizigo, ikiwa na kiraka cheupe.”

133 – Khalaf bin Saalim ametuhadithia: Wakiy´ ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa ´Amr bin Qays, ambaye amesema:

”´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) alionekana amevaa kikoi chenye viraka, akakemewa kwa vazi lake hilo, akasema: ”waumini wataiga kwa hili na moyo utanyenyekea kwa hili.”

134 – al-Fadhwl bin Sahl amenihadithia: Abu Nu´aym ametuhadithia: Sufyaan ametuhadithia, kutoka kwa al-Ajlah, kutoka kwa ´Abdullaah bin Abiyl-Hudhayl, ambaye amesema:

”Nilimuona ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) amevaa kanzu ya zamani sana iliyokuwa ikikaribia kuchakaa, ikiposhikiliwa ilifikia kucha na ikiachwa ilifika katikati ya mkono.”

[1] Abu Daawuud (4161). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (4161).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 167-177
  • Imechapishwa: 04/02/2026