Swali 19: Je, ukafiri wa Salaf kwa Jahmiyyah ulikuwa ukafiri mkubwa unaowatoa kwenye Uislamu au ulikuwa ukafiri mdogo uliokusudia kuonya na kukaripia tu?
Jibu: Takfiyr ya wanazuoni, maimamu na Salaf kwa Jahmiyyah ni ukafiri mkubwa unaowatoa kwenye Uislamu. ´Allaamah Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) ametaja kwamba wanazuoni 500 wamewakufurisha na akasema:
Hakika kheri ya wanazuoni khamsini pamoja na kumi,
walihukumu ukafiri wao katika miji tofauti.
Imaam al-Laalakaa´iy amesimulia ukafiri wao kutoka kwa wanazuoni, na alifanya hivo kabla yake at-Twabaraaniy
Wanazuoni wamesema kuwa Jahmiyyah wametoka kwenye yale mapote 72 ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema juu yake:
“Na ummah wangu utagawanyika katika makundi sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa kundi moja tu.”
Kutoka kwa Jahmiyyah kwenye makundi haya sabini na mawili kunamaanisha kwamba ukafiri wao ni ukafiri mkubwa, kwa sababu makundi haya sabini na mawili ni makundi ya Bid´ah ambayo yametishiwa Moto lakini hayajatoka kwenye Uislamu. Hata hivyo Jahmiyyah wametoka nje ya makundi haya sabini na mawili, pamoja na makundi mengine kama vile Qadariyyah waliochupa mipaka na pia Raafidhwah. Mapote haya matatu yametoka nje ya yale makundi sabini na mawili, kwa sababu Jahmiyyah wamekanusha majina na sifa za Allaah. Kukana majina na sifa husababisha kukanusha kuwepo kwa Allaah. Kitu kisicho na jina wala sifa hakiwezi kuwapo isipokuwa katika fikira za akili.
Vipi kinakuwa kitu kisichokuwa ndani ya ulimwengu, nje yake, kisichokuwa juu wala chini, kisichoambatana na ulimwengu wala kukamatana nao, kisicho na uwezo, hakisikii, hakioni, hakina uwezo, matakwa wala ujuzi? Hili ni jambo lisilowezekana. Kwa sababu hii ukafiri wao ni ukafiri mkubwa unaowatoa nje ya Uislamu.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 47-49
- Imechapishwa: 07/01/2026
Swali 19: Je, ukafiri wa Salaf kwa Jahmiyyah ulikuwa ukafiri mkubwa unaowatoa kwenye Uislamu au ulikuwa ukafiri mdogo uliokusudia kuonya na kukaripia tu?
Jibu: Takfiyr ya wanazuoni, maimamu na Salaf kwa Jahmiyyah ni ukafiri mkubwa unaowatoa kwenye Uislamu. ´Allaamah Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) ametaja kwamba wanazuoni 500 wamewakufurisha na akasema:
Hakika kheri ya wanazuoni khamsini pamoja na kumi,
walihukumu ukafiri wao katika miji tofauti.
Imaam al-Laalakaa´iy amesimulia ukafiri wao kutoka kwa wanazuoni, na alifanya hivo kabla yake at-Twabaraaniy
Wanazuoni wamesema kuwa Jahmiyyah wametoka kwenye yale mapote 72 ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema juu yake:
“Na ummah wangu utagawanyika katika makundi sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa kundi moja tu.”
Kutoka kwa Jahmiyyah kwenye makundi haya sabini na mawili kunamaanisha kwamba ukafiri wao ni ukafiri mkubwa, kwa sababu makundi haya sabini na mawili ni makundi ya Bid´ah ambayo yametishiwa Moto lakini hayajatoka kwenye Uislamu. Hata hivyo Jahmiyyah wametoka nje ya makundi haya sabini na mawili, pamoja na makundi mengine kama vile Qadariyyah waliochupa mipaka na pia Raafidhwah. Mapote haya matatu yametoka nje ya yale makundi sabini na mawili, kwa sababu Jahmiyyah wamekanusha majina na sifa za Allaah. Kukana majina na sifa husababisha kukanusha kuwepo kwa Allaah. Kitu kisicho na jina wala sifa hakiwezi kuwapo isipokuwa katika fikira za akili.
Vipi kinakuwa kitu kisichokuwa ndani ya ulimwengu, nje yake, kisichokuwa juu wala chini, kisichoambatana na ulimwengu wala kukamatana nao, kisicho na uwezo, hakisikii, hakioni, hakina uwezo, matakwa wala ujuzi? Hili ni jambo lisilowezekana. Kwa sababu hii ukafiri wao ni ukafiri mkubwa unaowatoa nje ya Uislamu.
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 47-49
Imechapishwa: 07/01/2026
https://firqatunnajia.com/19-takfiyr-ya-salaf-kwa-jahmiyyah-ni-kubwa-au-ndogo/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket