19. Hadiyth ”Nilimuona Mtume akiswali siku ya Ufunguzi wa Makkah… ”

Abu Daawuud (1/246) amesema: Musaddad ametuhadithia: Yahyaa bin Jurayj ametuhadithia: Muhammad bin ´Abbaad bin Ja´far amenihadithia, kutoka kwa Ibn Sufyaan, kutoka kwa ´Abdullaah bin as-Saa-ib, ambaye ameeleza:

”Nilimuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiswali siku ya Ufunguzi wa Makkah huku akiwa ameweka viatu vyake upande wa kushotoni mwake.”

Wanaume wa Hadiyth ni wanaume wa Swahiyh. Hadiyth imepokelewa pia na an-Nasaa’iy (2/58), Ibn Maajah (1/416), Ibn Abiy Shaybah (2/418), al-Haakim (1/259) na al-Bayhaqiy (2/432).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 20
  • Imechapishwa: 04/06/2025