Jambo la tatu ambalo ndiyo jawabu letu juu ya madai kwamba hali ya Hadiyth siyo ya kawaida, ni kwamba hali isiyo ya kawaida ina tafsiri mbalimbali. Mosi ni kwamba si yenye kuharibu Hadiyth kwa kila hali wala si jambo lililokubaliwa kwa makubaliano. an-Nawawiy amesema wakati alipokuwa akifafanua Hadiyth Swahiyh:
”Ni ile ambayo cheni yake imeungana kwa wapokezi waadilifu wenye kuhifadhi, bila ya kwenda kinyume wala dosari yoyote.”
as-Suyuutwiy amefafanua hilo na akasema:
”Imesemwa kwamba hakubainisha alichokusudia kwa kwenda kinyume hapa. Kumetajwa maoni matatu juu ya aina zake:
1 – Ni mpokezi mwenye kuaminika kumpinga aliye bora zaidi yake.
2 – Ni mpokezi mwenye kuaminika kupwekeka katika kusimulia.
3 – Ni mpokezi kupwekeka katika kusimulia.
Kauli mbili za mwisho zimekataliwa, hivyo dhahiri ni kwamba hapa alikusudia ya kwanza. Hili lina tatizo, kwa sababu ikiwa cheni imeungana na wapokezi wake wote ni waadilifu na madhubuti, basi kasoro zilizo wazi zimeondoka. Ikiwa imeondoka kuwa ni yenye dosari, basi ni nini kinachozuia kuhukumiwa kuwa ni Swahiyh? Kwa sababu tu mpokezi mmoja kumpinga aliye thabiti zaidi au walio wengi zaidi, hilo halilazimishi udhaifu, bali huwa ni katika mlango wa Swahiyh na iliyo Swahiyh zaidi… Pamoja na hayo sijaona yeyote katika maimamu wa Hadiyth wakishurutisha kuondoka kwa hali isiyo ya kawaida kwa maana ya upingano, bali kinachopatikana katika vitendo vyao ni kutanguliza baadhi ya riwaya juu ya nyingine katika kiwango cha usahihi.”[1]
Imaam an-Nawawiy amesema katika utafiti wa Hadiyth yenye hali isiyo ya kawaida:
“Ikiwa mpokezi hakumpinga mwingine kwa kupokea kwake peke yake, bali amepokea jambo ambalo wengine hawakulipokea, basi ikiwa ni mwadilifu, mwenye kuhifadhi na anayetegemewa katika uhifadhi wake, basi kule kupwekeka kwake ni sahihi. Na ikiwa hakuthibitishwa sana katika uhifadhi lakini hayuko mbali na daraja la watu madhubuti, basi alichojitokeza nacho ni nzuri. Ikiwa yuko mbali, basi ni yenye hali isiyo ya kawaida, inayopingana na yenye kukatawali.”
Haya yanafahamisha ya kwamba kwenda kinyume si dosari yenye kuharibu kwa kila hali, bali hukumu yake ni kwa mujibu wa ufafanuzi huu. Na kwamba aliye muadilifu, mwenye kuhifadhi na anayetegemewa katika uhifadhi wake, basi kule kupwekeka kwake katika kusimulia ni sahihi.
Miongoni mwa waliopinga wakaona kuwa hali isiyo ya kawaida kuwa ni kigezo cha kuharibu usahihi wa Hadiyth ni Imaam Ibn Daqiyq-il-´Iyd. al-´Iraaqiy amesema:
”Ama sharti la kusalimika na hali isiyo ya kawaida na dosari, Ibn Daqiyq-il-´Iyd amesema katika ”al-Iqtiraah”: ”Wapokezi wa Hadiyth wameongeza hilo katika ufafanuzi wa Swahiyh, jambo ambalo linahitaji kuangaliwa vyema kwa mujibu wa misingi ya wanazuoni wa Fiqh[2]. Kwa sababu dosari nyingi ambazo wanazuoni wa Hadiyth huzitaja kama kasoro haziwi kwa mujibu wa misingi ya wanazuoni wa Fiqh.” Ibn-us-Swalaah amesema: ”Huenda wakatofautiana katika kusahihisha Hadiyth kwa sababu ya kutofautiana kwao juu ya kuwepo kwa sifa hizi ndani yake au kwa sababu ya kutofautiana kwao katika kushurutisha baadhi yake.”
Hivyo tukapata faida kwamba kushurutisha kuslaimika kwa hali isiyo ya kawaida si jambo lililokubaliwa kwa makubaliano; bali ni jambo lenye makinzano. Kwa sababu hiyo Imaam al-Khattwaabiy amefafanua Hadiyth Swahiyh kuwa ni ”ile ambayo cheni yake imeungana na wapokezi wake ni waadilifu”. al-´Iraaqiy amesema kuhusu utambulisho huo:
”Hakushurutisha uhifadhi wa mpokezi, wala kusalimika na hali isiyo ya kawaida na dosari.”
Imesimuliwa kwamba masharti kama haya yanarejea katika ijtihadi ya wanazuoni katika kuchunguza riwaya. Kwa sababu hiyo vitabu vyao vya Hadiyth na yale waliyoyatoa vilitofautiana kwa kutofautiana kwa masharti yao, kama tulivyobainisha kwa upana katika utangulizi wa kitabu ”Hayaat-ul-Bukhaariy”. Kila kinachochunguzwa usahihi wake kwa kuzingatia cheni na kanuni za istilahi, basi hilo ni kwa upande wa kuzingatia usahihi wake kisanadi. Ama kuisahihisha kwa kuzingatia jambo la nje yake, nalo ndilo linaloitwa Swahiyh kupitia zingine, basi hiyo ni aina nyingine, kama utakavyokuja ubainifu wake.
[1] Tadriyb-ur-Raawiy, uk. 14-15.
[2]Wakazi wa Makkah ndio wanaojua zaidi njia na milima yake. Kwa hiyo kutegemea kunapaswa kuwa kwa wanazuoni wa Hadiyth, kwa sababu hii ni elimu yao waliobobea nayo, nao wanaifahamu zaidi kuliko wasiokuwa wao. Kila elimu hurejelewa kwa watu wa utaalamu na umahiri ndani yake. Wanazuoni wa Hadiyth wameafikiana juu ya kuweka sharti la Hadiyth Swahiyh kuwa salama na hali isiyo ya kawaida, kama ilivyo mashuhuri katika vitabu vyao. Na mwenye kufuatilia cheni za wapokezi katika vitabu vya Hadiyth basi atakuta si haba ya Hadiyth ambazo wapokezi waaminifu wamekhitalifiana katika kudhibiti matini zake khitilafu ambayo haiwezekani kuchukua nyuso zote za khitilafu hiyo kwa pamoja. Bali ni lazima kupendelea baadhi juu ya nyingine. Hivyo ile iliyo bora ndiyo iliyohifadhiwa, na ile iliyopungukiwa nguvu ndiyo isiyo ya kawaida – nayo ni miongoni mwa aina za Hadiyth dhaifu. Hadiyth ya kupangusa juu ya soksi ni Hadiyth Swahiyh iliyo na yenye kusalimika na hali isiyo ya kawaida, kama ilivyobainishwa hapo kabla. Kwa hiyo hakuna nafasi ya kuchukua tashwishi ya aliyekosea na kuituhumu Hadiyth kwa hali isiyo ya kawaida. Bali ni Hadiyth Swahiyh, iliyohifadhiwa na wanazuoni wa Hadiyth wameafikiana juu ya kusalimika kwake.
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 32-34
- Imechapishwa: 07/04/2026

Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 32-34
Imechapishwa: 07/04/2026
https://firqatunnajia.com/18-shubuha-ya-tatu-juu-ya-hadiyth-ya-al-mughiyrah-ni-yenye-hali-isiyo-ya-kawaida/