Aayah hii, ambayo ni Aayah Kursiy, ndio Aayah kubwa katika Qur-aan. Ndani yake mna uthibitisho na ukanushaji:

 الْحَيُّ الْقَيُّومُ

“… aliyehai daima, msimamia kila kitu.”

Huu ni uthibitisho:

لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ

“Haumchukuwi usingizi wala kulala.”

Huu ni ukanushaji:

لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ

“Ni Vyake pekee vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini.”

Huu ni uthibitisho.

مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ

“Nani huyu ambaye anashufai mbele Yake bila ya idhini Yake?”

Huu ni uthibitisho.

يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ

“Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao… ”

Huu ni uthibitisho.

وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ

“… wala hawawezi kuzunguka chochote katika ujuzi Wake isipokuwa kwa alitakalo. Kursiy Yake imeenea mbingu na ardhi wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo – Naye ni yujuu kabisa, ametukuka kabisa.” (02:255)

Amebainsiha ukamilifu Wake na kwamba Yeye ni ndiye aliye juu na mkuu na kwamba Yeye ana uhai kamili na kwamba Yeye ni aliye hai na kwamba ndiye msimamizi wa kila kitu na kwamba Yeye ndiye Mwenye kumiliki kila kitu. Lililo la wajibu ni kunyenyekea Kwake, kumuomba (Subhaanahu wa Ta´ala) na kumwelekea katika kila jambo. Mambo yote yanapitika kupitia mikono Yake. Ndio maana amesema (Subhaanah):

ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ

“Niombeni, Nitakuitikieni.” (40:60)

وَاسْأَلُوا اللَّـهَ مِن فَضْلِهِ

“Muombeni Allaah fadhilah Zake.” (04:32)

وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ

“Watakapokuuliza waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi niko karibu naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba.” (02:186)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 25-26
  • Imechapishwa: 19/10/2024