Jambo la pili ´Allaamah al-Maardiyniy amesema wakati akiraddi maneno ya al-Bayhaqiy kwamba ”hakuchukuliwi kitu kutoka kwa Abu Qays al-Awdiy wala Huzayl, pamoja na kupingana kwao na wakubwa waliopokea Hadiyth hii kutoka kwa al-Mughiyrah, waliotaja kupangusa juu ya soksi za ngozi”:
”Abu Daawud ameipokea na akainyamazia Hadiyth hii, Ibn Hibbaan akaisahihisha na at-Tirmidhiy akasema kuwa ni nzuri na Swahiyh. Ibn Ma´iyn amesema kuwa Abu Qays ´Abdur-Rahmaan bin Tharwaan ni mwenye kuaminika ilihali al-´Ijliy akasema kuwa ni mwenye kuaminika na thabiti. al-´Ijliy amesema pia kwamba Huzayl ni mwenye kuaminika ilihali al-Bukhaariy amepokea kutoka kwa wote wawili hao ndani ya ”as-Swahiyh” yake. Kisha wao hawakuwapinga watu kwa upingano unaokinzana, bali walipokea jambo la ziada juu ya walilolipokea wengine na kwa njia huru isiyopingana. Kwa hivyo hubebeshwa kuwa ni Hadiyth mbili tofauti. Kwa sababu hiyo Hadiyth ikasahihishwa, kama ilivyotangulia.”
Hivi divyo alivyosema ´Allaamah Aliy al-Qaariy katika ”Sharh-ul-Mishkaah”:
”Imesemekana kwamba kinachotambulika vyema katika riwaya ya al-Mughiyrah ni kupangusa juu ya soksi za ngozi. Jibu ni kwamba hakuna kizuizi kwa al-Mughiyrah kupokea matamko yote mawili, jambo ambalo limeungwa mkono na vitendo vya Maswahabah.”
Majina yao yatakuja baadaye na idadi yao kufikia Maswahabah kumi na sita.
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 31-32
- Imechapishwa: 07/04/2026
Jambo la pili ´Allaamah al-Maardiyniy amesema wakati akiraddi maneno ya al-Bayhaqiy kwamba ”hakuchukuliwi kitu kutoka kwa Abu Qays al-Awdiy wala Huzayl, pamoja na kupingana kwao na wakubwa waliopokea Hadiyth hii kutoka kwa al-Mughiyrah, waliotaja kupangusa juu ya soksi za ngozi”:
”Abu Daawud ameipokea na akainyamazia Hadiyth hii, Ibn Hibbaan akaisahihisha na at-Tirmidhiy akasema kuwa ni nzuri na Swahiyh. Ibn Ma´iyn amesema kuwa Abu Qays ´Abdur-Rahmaan bin Tharwaan ni mwenye kuaminika ilihali al-´Ijliy akasema kuwa ni mwenye kuaminika na thabiti. al-´Ijliy amesema pia kwamba Huzayl ni mwenye kuaminika ilihali al-Bukhaariy amepokea kutoka kwa wote wawili hao ndani ya ”as-Swahiyh” yake. Kisha wao hawakuwapinga watu kwa upingano unaokinzana, bali walipokea jambo la ziada juu ya walilolipokea wengine na kwa njia huru isiyopingana. Kwa hivyo hubebeshwa kuwa ni Hadiyth mbili tofauti. Kwa sababu hiyo Hadiyth ikasahihishwa, kama ilivyotangulia.”
Hivi divyo alivyosema ´Allaamah Aliy al-Qaariy katika ”Sharh-ul-Mishkaah”:
”Imesemekana kwamba kinachotambulika vyema katika riwaya ya al-Mughiyrah ni kupangusa juu ya soksi za ngozi. Jibu ni kwamba hakuna kizuizi kwa al-Mughiyrah kupokea matamko yote mawili, jambo ambalo limeungwa mkono na vitendo vya Maswahabah.”
Majina yao yatakuja baadaye na idadi yao kufikia Maswahabah kumi na sita.
Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 31-32
Imechapishwa: 07/04/2026
https://firqatunnajia.com/17-shubuha-ya-pili-juu-ya-hadiyth-ya-al-mughiyrah-inapingana-na-hadiyth-ya-kupangusa-juu-ya-soksi-za-ngozi/