Miongoni mwa alama za kutukuza maamrisho na makatazo ni kuwa mja asipitishe amri kwa sababu au kigezo kinachofanya kule kutii na kujisalimisha kwa amri ya Allaah (´Azza wa Jall) kudhoofika. Bali ajisalimishe kwa amri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na hukumu Yake hali ya kutekeleza kile alichoamrishwa nacho, ni mamoja iwe amejua hekima yake au hakujua. Akijua hekima ya uwekwaji Shari´ah ya amri au katazo, basi hilo limfanye azidishe utiifu na kujisalimisha na wala lisimfanye ajiondoe kwenye utekelezaji na kuacha amri hiyo, kama walivyofanya wengi wa wazandiki miongoni mwa wanaodai kuwa mafakiri na wanaojinasibisha na Suufiyyah.
Allaah (´Azza wa Jall) ameweka Shari´ah ya swalah tano ili kumuweka mja katika kukumbuka Kwake na kumtumia kwa moyo, viungo na ulimi katika ´ibaadah. Aidha kukipa kila kimojawapo haki yake katika utumwa wa ´ibaadah ambayo ndiyo sababu ya kuumbwa kwa mja. Hivyo swalah imewekwa juu ya ngazi kamilifu kabisa ya uja.
Hakika Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amemuumba huyu mwanaadamu na akamchagua kati ya viumbe wote na akaufanya moyo wake kuwa mahali pa hazina, upwekeshaji, ikhlaasw, mapenzi, haya, utukufu na uangalizi wa Allaah. Akafanya thawabu yake anapomjia iwe ni thawabu kamili zaidi na bora zaidi, nayo ni kuutazama uso Wake na kufanikishwa kwa radhi Zake na kuwa jirani Yake katika Pepo Yake.
Pamoja na hayo amemjaribu kwa matamanio, ghadhabu na kughafilika. aidha akamjaribu kwa adui yake Ibliys ambaye hamwachi kamwe. Hivyo humuingilia kupitia milango inayotokana na nafsi yake na tabia yake, na hivyo nafsi yake hutaka hayo, kwa sababu huingia kwake kwa yale anayoyapenda. Hivyo basi yeye, nafsi yake na matamanio yake hukusanyika dhidi ya mja. Watatu waliotawaliwa na wanaoamrisha. Huwatuma viungo vya mwili kutekeleza matakwa yao. Viungo vya mwili ni chombo kinachotii ambacho haviwezi isipokuwa kuitika. Hivi ndivyo hali ya hawa watatu na hali ya viungo, basi viungo haviachi kuwa katika utiifu wao wanapotoa amri na popote waelekezapo.
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 31-32
- Imechapishwa: 03/08/2025
Miongoni mwa alama za kutukuza maamrisho na makatazo ni kuwa mja asipitishe amri kwa sababu au kigezo kinachofanya kule kutii na kujisalimisha kwa amri ya Allaah (´Azza wa Jall) kudhoofika. Bali ajisalimishe kwa amri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na hukumu Yake hali ya kutekeleza kile alichoamrishwa nacho, ni mamoja iwe amejua hekima yake au hakujua. Akijua hekima ya uwekwaji Shari´ah ya amri au katazo, basi hilo limfanye azidishe utiifu na kujisalimisha na wala lisimfanye ajiondoe kwenye utekelezaji na kuacha amri hiyo, kama walivyofanya wengi wa wazandiki miongoni mwa wanaodai kuwa mafakiri na wanaojinasibisha na Suufiyyah.
Allaah (´Azza wa Jall) ameweka Shari´ah ya swalah tano ili kumuweka mja katika kukumbuka Kwake na kumtumia kwa moyo, viungo na ulimi katika ´ibaadah. Aidha kukipa kila kimojawapo haki yake katika utumwa wa ´ibaadah ambayo ndiyo sababu ya kuumbwa kwa mja. Hivyo swalah imewekwa juu ya ngazi kamilifu kabisa ya uja.
Hakika Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amemuumba huyu mwanaadamu na akamchagua kati ya viumbe wote na akaufanya moyo wake kuwa mahali pa hazina, upwekeshaji, ikhlaasw, mapenzi, haya, utukufu na uangalizi wa Allaah. Akafanya thawabu yake anapomjia iwe ni thawabu kamili zaidi na bora zaidi, nayo ni kuutazama uso Wake na kufanikishwa kwa radhi Zake na kuwa jirani Yake katika Pepo Yake.
Pamoja na hayo amemjaribu kwa matamanio, ghadhabu na kughafilika. aidha akamjaribu kwa adui yake Ibliys ambaye hamwachi kamwe. Hivyo humuingilia kupitia milango inayotokana na nafsi yake na tabia yake, na hivyo nafsi yake hutaka hayo, kwa sababu huingia kwake kwa yale anayoyapenda. Hivyo basi yeye, nafsi yake na matamanio yake hukusanyika dhidi ya mja. Watatu waliotawaliwa na wanaoamrisha. Huwatuma viungo vya mwili kutekeleza matakwa yao. Viungo vya mwili ni chombo kinachotii ambacho haviwezi isipokuwa kuitika. Hivi ndivyo hali ya hawa watatu na hali ya viungo, basi viungo haviachi kuwa katika utiifu wao wanapotoa amri na popote waelekezapo.
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 31-32
Imechapishwa: 03/08/2025
https://firqatunnajia.com/17-jisalimisha-na-maamrisho-na-makatazo-kwa-hali-zote/