17. Hadiyth kwa mapokezi mengi kuhusu kusuniwa kuswali na viatu

Yanatosha haya. Nimeacha Hadiyth zingine nyingi zinazofahamisha uwekwaji Shari´ah wa kupangusa juu ya viatu ikiwa ni pamoja na katika “Majma´-uz-Zawaa’id” na “al-Musannaf” ya ´Abdur-Razzaaq, kwa sababu ya usahihi wake ingawa baadhi yazo zinafaa kutumiwa kwa lengo la kutilia nguvu na ufuatiliaji. Khaswa ukizingatia kuwa at-Twahaawiy amesema kuwa Hadiyth zinazojulisha kufaa kuswali na viatu zimepokelewa kwa mapokezi tele. Amesema:

”Kumesimuliwa Hadiyth nyingi mno kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) zinazoonyesha kuwa kuswali na viatu ni jambo limewekwa katika Shari´ah. Zinafahamisha kuanzia kwamba yeye mwenyewe (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali na viatu vyake na akavua viatu vyake kwa sababu ya uchafu, mpaka kuruhusu kuswali na viatu.”[1]

Wanazuoni hawashurutishi kuwa kila njia ya Hadiyth iwe Swahiyh au nzuri ili Hadiyth izingatiwe kuwa imepokelewa kwa mapokezi mengi. Bali wanajumuisha zilizokuwa Swahiyh,  nzuri na dhaifu.

[1] Ma´aaniyl-Aathaar (1/511).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 17
  • Imechapishwa: 03/06/2025