17. Dalili juu ya mkono wa Allaah 3

17- Abul-Fadhwl Ja´far bin Muhammad bin Ya´quub as-Sandaliy ametuhadithia: al-Hasan bin Muhammad ametuhadithia: Shabaabah ametuhadithia: Warqaa´ ametuhadithia, kutoka kwa Abuz-Zinaad, kutoka kwa al-A´raj, kutoka kwa Abu Hurayrah ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Pindi Allaah (´Azza wa Jall) alipoumba viumbe akaandika kwenye kitabu kilichoko Kwake juu ya ´Arshi: “Huruma yangu inashinda ghadhabu Zangu.”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 52-53
  • Imechapishwa: 05/11/2017