Pindi Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) na watunzi wengine waliotunga vitabu vya ´Aqiydah wanapokataza mijadala na magomvi, malengo yao ni ile mijadala isiyokuwa na faida na haja. Bali inapelekea tu Ahl-ul-Bid´ah kufuatwa, jambo ambalo halifai katika dini ya Allaah kwa ujumla na khaswa katika maudhui makubwa kama haya. Haitakiwi kujadili kuhusu Qadar, waumini kumuona Mola wao Peponi na mfano wa hayo. Haki inatakiwa kubainishwa katika mambo haya na kufanya kama alivosema Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
وَقُلِ الْحَقُّ مِن رَّبِّكُمْ ۖ فَمَن شَاءَ فَلْيُؤْمِن وَمَن شَاءَ فَلْيَكْفُرْ
”Sema: ”Hii ni haki kutoka kwa Mola wenu; hivyo basi yule anayetaka aamini na yule anayetaka akufuru.”[1]
Pindi Sunnah itapobainika kutokamana na Bid´ah, yule anayetaka kushikamana na Sunnah afanye hivo, jambo ambalo ni kheri kwake, na yule anayetaka kushikamana na Bid´ah za Motoni na mifumo ya wapotevu basi ameidhulumu nafsi yake mwenyewe. Amejikosesha mwenyewe Sunnah tukufu na yale yote yanayopelekea kwayo katika thawabu nyingi. Huu ndio upambanuzi ninaoweza kukumbuka kwa sasa.
[1] 18:29
- Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 69
- Imechapishwa: 08/10/2019
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)