116 – ´Abdullaah bin Abiy Badr ametuhadithia: Shu´ayb bin Harb ametukhabarisha: Swaalih al-Murriy ametuhadithia:
”Alitoka al-Hasan, Yuunus na Ayyuub na huku wakikumbushana kuhusu unyenyekevu. al-Hasan akawaambia: “Je, mnajua unyenyekevu ni nini? Unyenyekevu ni kutoka nyumbani kwako na usikutane na muislamu yeyote isipokuwa umuone kuwa ni mbora kuliko wewe.”
117 – Ishaaq bin Ibraahiym ametuhadithia: Abu Yaziyd ar-Raaziy ametuhadithia: Ishaaq bin Ibraahiym bin Yaziyd ametuhadithia: Maslamah bin Ja´far ametuhadithia, kutoka kwa Sa´d at-Twaa’iy, aliyeeleza kwamba Iysaa bin Maryam (´alayhis-Salaam) amesema:
”Twubaa kwa wanyenyekevu duniani, hao ndio wenye viti vya nuru siku ya Qiyaamah. Twubaa kwa wanaotengeneza baina ya watu duniani, hao ndio warithi wa al-Firdaws siku ya Qiyaamah. Twubaa kwa waliotwaharika nyoyo zao duniani, hao ndio wataomuona Allaah (´Azza wa Jall) siku ya Qiyaamah.”
118 – Ahmad bin Hanbal ametuhadithia: ´Abdullaah bin al-Mubaarak ametukhabarisha: al-Mas´uudiy ametukhabarisha, kutoka kwa Yahyaa bin Kathiyr, ambaye amesema:
“Asili ya unyenyekevu ni mambo matatu: Kuridhika na sehemu ya chini ya kikao, kuanza kwa salamu kwa yule unayekutana naye na kuchukia kusifiwa na kujionyesha kwa wema.”
119 – Kwa njia hiyohiyo ametukhabarisha Ma´mar: Yuunus bin Khabbaab amenikhabarisha, kutoka kwa Mujaahid, ambaye amesema:
“Hakika Allaah (´Azza wa Jall) alipowazamisha watu wa Nuuh, basi milima ilijivuna na mlima al-Juwdiy ukanyenyekea, Allaah akauinua juu ya milima na akaufanya kuwa ndio mahala pa kupumzika kwa safina.”
120 – Kutokea huko ametuhadithia Hamzah bin Najiyd, kutoka kwa Salamah bin Abiy Habiyb, kutoka kwa ´Abdullaah bin al-Hasan, ambaye ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Anayenyenyekea Allaah humuinua, anayejivuna Allaah humvunja, anayejitegemea Allaah humtajirisha, anayebadhirisha Allaah humfakirisha na anayemtaja Allaah (´Azza wa Jall) Allaah humpenda.”[1]
121 – Kwa njia hiyohiyo ametuhadithia Zakariyyaa bin ´Adiy, kutoka kwa Yahyaa bin Sulaym at-Twaa’iy, kutoka kwa Muhammad bin ´Abdillaah bin ´Amr bin ´Uthmaan: Nimefikiwa ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Anapomuongoza Allaah kwa Uislamu mja, akapendezesha sura yake, akamweka katika nafasi isiyomfedhehesha na akamruzuku pamoja na hayo unyenyekevu, basi huyo ni miongoni mwa waliochaguliwa na Allaah (´Azza wa Jall).”
122 – Muhammad bin ´Abdillaah bin Muusa amenihadithia: Zayd bin Hubaab ametuhadithia, kutoka kwa Shu´bah, kutoka kwa ´Aliy bin Zayd, kutoka kwa Anas bin Maalik, ambaye amesema:
“Hakika kijakazi wa mjini Madiynah alikuwa akimshika mkono Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) naye hasiti kuufuta mkono wake mpaka ampeleke popote apendapo.”[2]
[1] al-Haythamiy amesema:
“Kwa njia hiyohiyo nazitambua mbili tu.” (Madjma´-uz-Zawaa’id (10/253))
[2] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Ibn Maajah” (3386).
- Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 152-158
- Imechapishwa: 04/02/2026

Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 152-158
Imechapishwa: 04/02/2026
https://firqatunnajia.com/17-asili-ya-unyenyekevu-ni-mambo-matatu/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket