Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
134 – Tunaona kufaa kufuta juu ya soki za ngozi, ni mamoja wakati wa safari na mjini. Hivyo ndivyo imepokelewa.
MAELEZO
Kwa nini ametaja mambo haya ya tanzu katika kitabu cha ´Aqiydah? Kwa sababu mambo haya wameyapinga wazushi. Ahl-us-Sunnah wameyathibitisha kutokana na Hadiyth nyingi zilizopolewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Raafidhwah ndio wanaotambulika zaidi kupinga kupangusa juu ya soksi za ngozi. Wanaenda kinyume na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah katika jambo hilo. Wanaenda kinyume na Hadiyth zilizothibiti. Kupangusa kumethibiti; mchana mmoja na usiku wake kwa ambaye ni mwenyeji na michana mitatu na nyusiku zake kwa ambaye ni msafiri. Hii ni ruhusa na wepesi kutoka kwa Allaah juu ya waja Wake.
Raafidhwah wanapinga kupangusa juu ya soksi za ngozi. Badala yake wanajuzisha kupangusa juu ya miguu, jambo ambalo ni kosa kubwa kabisa. Hakuna yeyote anayesema kupangusa juu ya miguu. Namna hii pindi walipoamua kuiacha haki ndipo Allaah akawapa mtihani wa batili.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 184
- Imechapishwa: 04/12/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)