Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
133 – Katika yale ambayo hatuna uhakika nayo tunasema “Allaah ndiye mjuzi zaidi”.
MAELEZO
Hili ni jambo kubwa – suala la elimu. Mtu hatakiwi kusema asichokijua. Akijua kitu, basi akiseme. Akiwa hana ujuzi juu ya kitu, asikiseme. Asizungumze kitu juu ya mambo ya dini na mambo ya ´ibaadah na wala asijiingize ndani yake pasi na elimu. Bali anatakiwa kusimama na kusema “Allaah ndiye mjuzi zaidi”. Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) siku moja aliulizwa maswali arobaini ambapo akajibu maswali manne. Akasema kuhusu maswali yaliyosalia:
“Sijui.”
Muulizaji akamweleza kuwa amekuja juu ya ngamia kutokea nchi ya mbali na akamuuliza ni namna gani anashindwa kumjibu maswali yake. Ndipo Imaam Maalik akamwambia mtu yule apande ngamia wake na arudi katika nchi yake na awatangazie watu kuwa amemuuliza Maalik ambapo akajibu:
“Sijui.”
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa anaulizwa kitu ambacho hajateremshiwa Wahy, basi anasubiri mpaka pale atakapofunuliwa Wahy. Pindi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa anawauliza Maswahabah kitu wasichokijua, walikuwa wakijibu:
“Allaah na Mtume Wake ndio wanajua zaidi.”
Hawabahatishi. Ni muhimu sana kutambua jambo hili. Allaah (´Azza wa Jall) amefanya kusema juu Yake pasi na elimu ngazi yake ni khatari zaidi kuliko shirki pale aliposema:
قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَالْإِثْمَ وَالْبَغْيَ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَأَن تُشْرِكُوا بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ
“Sema: “Hakika si vyenginevyo Mola wangu ameharamisha machafu, yaliyodhihirika na yaliyofichika na dhambi [aina zote] na ukandamizaji bila ya haki na [ameharamisha] kumshirikisha Allaah kwa ambayo hakukiteremshia mamlaka na kuzungumza juu ya Allaah yale ambayo hamyajui.”[1]
وَلاَ تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ
“Na wala usiyafuate yale usiyokuwa nayo elimu.”[2]
Ndugu! Inakutosha kusema kuwa hujui. Mwenye kusema kuwa hajui amejibu. Usibahatishe. Usijiingize ndani ya hukumu za dini pasi na elimu. Hushuki ngazi kwa kusema kuwa hujui yale usiyoyajua. Kinyume chake. Ni sifa kamilifu, kwa sababu ni kujichunga na ni kumcha Allaah, jambo ambalo watu watakusifu kwacho.
Hii leo, ambapo wasomaji wamekuwa wengi na wanazuoni wamekuwa wachache, kuna watu wengi wanaojinasibisha na elimu ambao wanatoa fatwa, wanahukumu na wanaziparamia hukumu za Shari´ah katika vyombo vya mawasiliano na kwenginepo pasi na elimu. Kutokana na fadhilah za Allaah ujinga wao umefichuka mbele ya watu. Allaah amewafedhehesha. Ingelikuwa vyema kwao – mbele ya Allaah na mbele ya watu – endapo wangezisitiri nafsi zao na wakasimama katika yale wasiyokuwa na elimu kwayo. Hebu tuzingatie jambo hili.
[1] 7:33
[2] 17:36
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 182-184
- Imechapishwa: 04/12/2024

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 182-184
Imechapishwa: 04/12/2024
https://firqatunnajia.com/168-usibahatishe-katika-uislamu/