Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
130 – Hatuondoi mkono katika kuwatii. Tunaona kuwa kuwatii wao ni kumtii Allaah (´Azza wa Jall) ambako amefaradhisha muda wa kuwa hawajaamrisha maasi. Tunawaombea kutengemaa na kusalimika.
MAELEZO
Huku ni kutilia mkazo yale yaliyotangulia. Hata kama watadhulumu, watanyanyasa, watafanya maasi na madhambi makubwa yasiyokuwa shirki, sisi hatutosimamisha kuwatii. Hatutofanya uasi dhidi yao na wala hatutowaasi:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ
“Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi.”[1]
Bali tunapambana jihaad bega kwa bega tukiwa nao na tunashuhudia swalah za ijumaa, swalah za mkusanyiko na swalah za ´iyd pamoja nao kwa ajili ya umoja wa waislamu. Allaah (Ta´ala) ametuamrisha kuwatii watawala waislamu kinyume na watawala wa kikafiri:
وَلَن يَجْعَلَ اللَّـهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلًا
“… na Allaah hatojaalia kwa makafiri njia [ya kuwashinda] dhidi ya waumini.”[2]
Kwa sababu sentesi isemayo:
وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ
“… na wenye madaraka katika nyinyi.”
inawakusudia waislamu. Mtawala wa waislamu anapaswa kutiiwa katika yale yasiyohusiana maasi. Mtawala akiamrisha maasi, basi usimtii katika maasi hayo. Lakini haina maana kwamba umfanyie uasi na umuasi katika mambo mengine yote. Bali usimtii katika maasi hayo tu. Mtii katika mengine yote. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.”[3]
Tunamuomba Allaah awarudishe watawala katika haki na asahihishe yale makosa walionayo. Tunawaombea kutengemaa. Kutengemaa kwao ndio kutengemaa kwa waislamu. Kuongoka kwao ndio kuongoka kwa waislamu. Manufaa yao yanawaenea wengine. Kwa hivyo ukiwaombea wao, umewaombea waislamu.
[1] 4:59
[2] 4:141
[3] al-Bukhaariy (7258) na Muslim (1840).
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 173-174
- Imechapishwa: 01/12/2024
Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
130 – Hatuondoi mkono katika kuwatii. Tunaona kuwa kuwatii wao ni kumtii Allaah (´Azza wa Jall) ambako amefaradhisha muda wa kuwa hawajaamrisha maasi. Tunawaombea kutengemaa na kusalimika.
MAELEZO
Huku ni kutilia mkazo yale yaliyotangulia. Hata kama watadhulumu, watanyanyasa, watafanya maasi na madhambi makubwa yasiyokuwa shirki, sisi hatutosimamisha kuwatii. Hatutofanya uasi dhidi yao na wala hatutowaasi:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ
“Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi.”[1]
Bali tunapambana jihaad bega kwa bega tukiwa nao na tunashuhudia swalah za ijumaa, swalah za mkusanyiko na swalah za ´iyd pamoja nao kwa ajili ya umoja wa waislamu. Allaah (Ta´ala) ametuamrisha kuwatii watawala waislamu kinyume na watawala wa kikafiri:
وَلَن يَجْعَلَ اللَّـهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلًا
“… na Allaah hatojaalia kwa makafiri njia [ya kuwashinda] dhidi ya waumini.”[2]
Kwa sababu sentesi isemayo:
وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ
“… na wenye madaraka katika nyinyi.”
inawakusudia waislamu. Mtawala wa waislamu anapaswa kutiiwa katika yale yasiyohusiana maasi. Mtawala akiamrisha maasi, basi usimtii katika maasi hayo. Lakini haina maana kwamba umfanyie uasi na umuasi katika mambo mengine yote. Bali usimtii katika maasi hayo tu. Mtii katika mengine yote. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.”[3]
Tunamuomba Allaah awarudishe watawala katika haki na asahihishe yale makosa walionayo. Tunawaombea kutengemaa. Kutengemaa kwao ndio kutengemaa kwa waislamu. Kuongoka kwao ndio kuongoka kwa waislamu. Manufaa yao yanawaenea wengine. Kwa hivyo ukiwaombea wao, umewaombea waislamu.
[1] 4:59
[2] 4:141
[3] al-Bukhaariy (7258) na Muslim (1840).
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 173-174
Imechapishwa: 01/12/2024
https://firqatunnajia.com/161-kiongozi-mwema-huzalisha-raia-wema/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)