160. al-Qummiy upotoshaji wake wa nne wa al-Anfaal

al-Qummiy ametaja cheni yake ya wapokezi hadi kwa Abu Ja´far ambaye amesema kuhusiana na maneno Yake (Ta´ala):

إِنَّ شَرَّ الدَّوَابِّ عِندَ اللَّـهِ الَّذِينَ كَفَرُوا فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ

”Hakika viumbe waovu kabisa mbele ya Allaah ni wale waliokufuru nao hawaamini.”[1]

“Aayah hii iliteremshwa juu ya Banuu Umayyah. Wao ni viumbe waovu kabisa wa Allaah. Hao ndio waliokufuru katika maana ya undani wa Qur-aan. Hivyo hawaamini.”[2]

Allaah amemtakasa Abu Ja’far kutokana na upotoshaji huu wa Baatwiniy. Mada ya Aayah inawahusu makafiri. Miongoni mwa waovu zaidi ni Baatwiniyyah wenye chuki dhidi ya Uislamu na wanapotosha Kitabu cha Allaah. Wao ni waovu zaidi miongoni mwa makafiri na wenye madhara zaidi juu ya Uislamu na waislamu. Hawana chuki dhidi ya Banuu Umayyah kwa jengine isipokuwa tu ni kwa sababu Allaah aliutukuza Uislamu na wakawatweza waabudia, mayahudi na manaswara chini ya ukhaliyfah wao. Banuu Umayyah walikuwa waislamu. Miongoni mwao kulikuwa na Maswahabah bora waliokuwa viongozi hodari katika jihaad na kufanikisha funguzi. Walikuwa ni wafalme wa kiislamu ambao walifikia ufunguzi wa miji mingi Mashariki na Magharibi. Dini na katiba yao ilikuwa Uislamu na hawakuwa wanataka kitu kingine badala yake. Miongoni mwao wako ambao ni madhalimu, hata hivyo walikuwa wakijifakharisha kwa Uislamu.

[1] 8:55

[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/279).

  • Muhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 219-220
  • Imechapishwa: 13/08/2025